Meek Mill Azua Gumzo Mitandaoni Baada ya Tweets Zenye Msimamo Mkali

Meek Mill Azua Gumzo Mitandaoni Baada ya Tweets Zenye Msimamo Mkali

Msanii maarufu wa hip hop Meek Mill amezua gumzo mtandaoni baada ya kuchapisha mfululizo wa tweets zenye ujumbe mzito kuhusu shutuma mbalimbali, maisha ya anasa, na heshima ya jina lake. Katika ujumbe wake, Meek Mill amekanusha vikali madai kwamba aliwahi kushambuliwa au kuibiwa, akieleza kuwa alipokuwa Los Angeles alikutana na watu mashuhuri kama Suge Knight na Big U bila hofu yoyote. Anasema lengo lake lilikuwa kuonyesha vijana kuwa kuna maisha zaidi ya vurugu, hasa kwa jamii ya Weusi.  “Luce Cannon na kile kikao chake na Akademiks kilikuwa mtego mtupu… halafu huyu mtu hana jina, anasema eti alinivamia na kunipora.” Akaongeza: “Nilikuwa nakutana na Suge Knight na Big U nilipokuwa LA… bila kamera wala mbwembwe!” Akisisitiza kuwa madai ya kushambuliwa ni ya uongo. Meek pia ameeleza kutoridhishwa na mazingira ya sherehe za mastaa, akidai kuwa matumizi ya dawa za kulevya, hasa “coke”, ni jambo la kawaida. Hata hivyo, anasisitiza kuwa yeye hajawahi kulewa hata bangi na anaepuka utegemezi wa vitu hivyo licha ya kuwa na utajiri mkubwa tangu akiwa na miaka 23. “Kitu cha kushangaza zaidi nilichowahi kuona kwenye sherehe ya Puff ni ‘vibes za coke’… na hii hutokea kwenye hizi sherehe zote.” Akasisitiza msimamo wake kwa kusema: “Nimekuwa na mamilioni tangu nikiwa na miaka 23, sitaki hata kuwa mraibu wa bangi… Sihukumu, lakini naona mambo kwa jicho tofauti!” Aidha, amekosoa baadhi ya blogu kwa kumhusisha na kesi ya Lil Rod dhidi ya Diddy, akisema kuwa jina lake halikutajwa lakini mitandao imejaribu kumchafua. Anasisitiza kuwa jamii yake haikuamini tuhuma hizo, lakini bado ni shambulio dhidi ya chapa yake. “Wakati Diddy anakabiliwa na kesi ya FEDERAL, nataka kuibua tena suala la Lil Rod na kesi yake ambayo ilitupiliwa mbali. Hakuwahi kutaja jina langu, lakini blogu ziliendeleza ajenda nzima dhidi yangu.” Akaongeza: “Jamii yangu haikuamini lakini hii ni hujuma dhidi ya chapa yangu… nataka kujua ukweli wa yote haya!” Kauli hizi kutoka kwa Meek Mill zimezua hisia mseto miongoni mwa mashabiki na watumiaji wa mitandao ya kijamii. Baadhi wamempongeza kwa uwazi wake na msimamo thabiti, huku wengine wakimtaka awe makini na kauli zake, hasa wakati huu ambapo kesi ya Diddy bado iko kwenye mchakato wa kisheria.

Read More
 Rapa Meek Mill awaomba radhi wananchi wa Ghana

Rapa Meek Mill awaomba radhi wananchi wa Ghana

Rapa Meek Mill amewaomba msamaha wananchi wa Ghana baada ya kuonesha kutokupendezwa na video yake ijayo ambayo kuna vipande amevirekodia katika Ikulu ya Ghana. Meek Mill kupitia ukurasa wake wa Twitter amedai kuwa nia yake ni kuunganisha Wamerekani weusi na waafrika huku akisema kuwa hakujua tamaduni za Kiafrika. “My apologies to the people if any disrespect! We still gonna push to make the connection between black people in America and Africa … what I’m trying to do is more than a video and you should see coming soon! My apologies to the the office also!”, Aliandika.

Read More
 Meek Mill atangaza kutua barani Afrika kwa mara ya pili

Meek Mill atangaza kutua barani Afrika kwa mara ya pili

Rapa kutoka nchini Marekani Meek Mill ametangaza kurudi tena barani Afrika kwa mara ya pili baada ya kutua kwa mara ya kwanza nchini Ghana kwenye tamasha la Afro Nation lililofanyika mwishoni mwa mwaka 2022 Meek ametoa taarifa kupitia ukurasa wake wa twitter kuwa anatarajia kutua nchini Nigeria muda wowote kuanzia sasa. “Nakuja Nigeria”, Aliandika. Lakini pia Rapa huyo amefunguka kuwa anahitaji msambazaji wa kazi zake Barani Afrika na Uingereza. Si hivyo tu Meek amesisitiza kuwa Afrika ni Bara kubwa zaidi duniani, inabidi watu tujiunge kwa pamoja

Read More
 Meek Mill awatoa jela wanawake 20 huko Philadelphia

Meek Mill awatoa jela wanawake 20 huko Philadelphia

Rapa Meek Mill ambaye alizaliwa na kukulia mjini Philadelphia, Marekani ameamua kurudisha fadhila kwao. Rapa huyo ameripotiwa kuwatoa wanawake 20 jela huko Philadelphia kwa kuwalipia dhamana zao. Lengo la Meek Mill kufanya hivyo, ni kuhakikisha kuwa wanarudi nyumbani kufurahia sikukuu na familia zao. Katika taarifa kwa vyombo vya habari Meek Mill amesema “Ilikuwa ni huzuni kwangu kuwa mbali na mwanangu katika kipindi cha sikukuu wakati nilipokuwa jela…hivyo ninaelewa wanachopitia wanawake hawa na familia zao, hakuna mtu anayepaswa kukaa gerezani kwa sababu tu hana uwezo wa kulipa dhamana. “Nashukuru kupata nafasi ya kuwasaidia wanawake hawa kuwa pamoja na familia zao katika msimu huu maalum wa mwaka” Tayari wanawake 5 wameachiwa kutoka jela lakini 15 wengine wanatajwa kuachiwa huru wiki ijayo.

Read More
 Rapa Meek Mill ajitoa kwenye mtandao wa Twitter

Rapa Meek Mill ajitoa kwenye mtandao wa Twitter

Rapa Meek Mill ametangaza kuachana na mtandao wa Twitter baada ya kuweka wazi rasmi kuifuta akaunti yake ya mtandao huo. Sababu kubwa hasa ya Meek Mill kufikia maamuzi hayo amebainisha kuwa, mtandao huo una utaratibu na watu wa ajabu mno na sasa atakuwa akiutumia zaidi mtandao wa YouTube. “Nimeamua kuiondoa akaunti yangu ya Twitter jumla na nitatumia mitandao mingine ya kijamii yenye hali nzuri ikiwa na lengo la kujenga, na hata kutia motisha. Kwa hiki ambacho kinaendelea upande wa Twitter kimepelekea nichukue maamuzi hayo.”  Unasomeka ujumbe wa Meek Mill kabla hajaifuta akaunti yake hiyo. “Nitakuwa nikitumia akaunti yangu ya YouTube badala ya Twitter kwa ajili ya kuendelea kuwa karibu na watu wangu”, Alitweet Meek Mill.

Read More
 MEEK MILL KUTOA MSAADA WA SHILLINGI MILLIONI 56.7 MSIMU HUU WA SIKUKUU MJINI KWAO PHILADELPHIA

MEEK MILL KUTOA MSAADA WA SHILLINGI MILLIONI 56.7 MSIMU HUU WA SIKUKUU MJINI KWAO PHILADELPHIA

Rapa kutoka nchini Marekani Meek Mill anarudisha fadhila kwao, tovuti ya TMZ imeripoti kwamba rapa huyo atatumia zaidi ya shillingi milllioni 56.7 za Kenya kwa ajili ya kutoa zawadi pamoja na mahitaji mengine mbali mbali kwa familia zenye uhitaji mjini kwao Philadelphia msimu huu wa Sikukuu. Meek Mill ambaye alizaliwa na kukulia Philadelphia amepanga kutoa zawadi kibao zikiwemo Pikipiki, Video game gift cards, Laptops, tablets, midoli na zawadi nyingine kibao. Aidha imeelezwa kwamba atasindikizwa na washirika wake wakubwa; Robert Kraft na Michael Rubin pia mameneja wake toka Roc Nation.

Read More