Mejja awaonya mashabiki dhidi ya matapeli mtandaoni

Mejja awaonya mashabiki dhidi ya matapeli mtandaoni

Staa wa muziki nchini Mejja ametoa angalizo kwa mashabiki zake kuwa makini na baadhi ya matapeli wa mitandao wanaotumia jina lake kujitakia makuu. Kupitia instastory yake,Hitmaker huyo wa “Usiniharibie Mood” amewaonya mashabiki kwamba hausiki kwa chochote na wala hatowajibika kwa watu wasio waaminifu wanaojifanya kuwa yeye. Aidha amesema hajawahi kuwa na akaunti yeyote kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook, Twitter na Tiktok huku akisisitiza kuwa mtandao pekee ambao ana umiliki wa akaunti ni Instagram. Mejja ametoa kauli hiyo mara baada ya mtumiaji mmoja wa Facebook anayetumia jina lake kuchapisha taarifa ya kumpongeza msanii Trio Mio ambaye kwa mujibu wa akaunti hiyo alipata alama ya D- kwenye mtihani wa KCSE.

Read More
 Mejja ataka bangi kuhalalishwa Kenya

Mejja ataka bangi kuhalalishwa Kenya

Mwanamuziki nyota nchini Mejja ametaka serikali kuhalalisha kilimo cha mimea wa bangi kwa manufaa ya taifa. Kwenye mahojiano na Plug tv Hitmaker huyo wa Kanairo Dating amesema licha ya bangi kuwa na mitazamo hasi katika jamii, serikali inapaswa kuja na mkakati wa kuhakikisha kuwa zao hilo linazalisha pato la taifa. Kauli ya mejja imekuja mara baada ya Rapa Octopizzo miezi miwili iliyopita kumtaka Rais William Ruto kuihalalisha bangi pindi tu atakapokula kiapo cha kuingia ofisini kama Rais wa tano wa Kenya. Katika video ambayo ilisambazwa mitandaoni, Octopizzo alimuelezea Ruto kwamba hata kama ataona kuhalalisha bangi ni jambo gumu basi aifanye isiwe kama ni hatia kwa mtu anayepatikana naye bali liwe tu ni jambo la kawaida. “Najua wewe ni mkristo na kwa hiyo hili gumzo huenda litakuwa gumu kidogo kwako lakini unajua bangi ni moja ya dawa ambazo ni takatifu zaidi duniani. Na amabcho nakuomba hata si kuhalalisha matumizi yake bali ni kuiweka bangi isiwe kama hatia kwa mtu anayepatikana nayo,” alisema Octopizzo. “Juzi nilikuona ulikutana na seneta wa Delaware, huko mtu anaruhusiwa kutembea na bangi gramu 3 kwa kujivinjari tu ilmradi mtu ako na miaka 21. Hii ni biashara ya mabilioni na tunajua kuna watu serikalini wenye wanafanya biashara hiyo,” Staa huyo alisema.

Read More
 Mejja ahapa kutoanika mahusiano yake kwenye mitandao ya kijamii

Mejja ahapa kutoanika mahusiano yake kwenye mitandao ya kijamii

Staa wa muziki nchini Mejja amefunguka kuwa hatokuja kuweka wazi mahusiano yake kwenye mitandao ya kijamii. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni hitmaker huyo wa “Kanairo Dating” amesema ameamua kuchukua hatua hiyo kwa sababu mahusiano yake ya nyuma yalikumbwa na mikosi kutokana yeye kuanika mtandaoni. Mejja ambaye amethibitisha kuwa kwenye mahusiano mapya ya kimapenzi amesema hana mpango wa kumchumbia mtu maarufu hasa msanii mwenzake kwani mastaa wengi huwa hayadumu kwenye mahusiano. Utakumbuka Mejja alikuwa kwenye mahusiano na mrembo aitwaye Milly Wairimu lakini walikuja wakaachana kwa madai ya usaliti.

Read More
 MEJJA AMJIBU EX WAKE MILLY WAIRIMU

MEJJA AMJIBU EX WAKE MILLY WAIRIMU

Staa wa muziki nchini Mejja amefunguka kuhusu suala la mpenzi wake wa zamani Milly Wairimu kuzungumzia vibaya kwenye mitandao ya kijamii. Kupitia mahojiano na Nicholas Kioko amesema hana muda wa kupishana na ex wake huyo kwa kuwa ana mambo mengi muhimu anayojishughulisha nayo. Kuhusu ishu ya kubeba tumbler kwenye nyimbo zake, Mejja amesema alipata wazo la kubeba tumbler hiyo baada ya kugundua kuwa kuna mchekeshaji mmoja kwenye mitandao ya kijamii alikuwa anatumia video zake akiwa amebeba tumbler kwenye video zake za ucheshi. Hitmaker  huyo wa “Kanairo Dating” ametangaza mpango wa kugeuza tumbler kuwa biashara kwani amekuwa na mpango wa kuanza kuzalisha na kuuza tumbler kwa bei nafuu kwa wakenya. Mbali na hayo Mejja ameamua kumpa Clemmo maua yake akiwa hai kwa kusema kuwa mhasisi huyo wa Carlif Records ndiye alimkingia kifua kipindi anaanza muziki yaani alimpa malazi, chakula na kumsaidia kimuziki na ndio maana huwa anamtaja sana kwenye nyimbo zake. Pia ametupasha mapya kuhusu maendeleo ya album yake mpya kwa kusema kuwa ilipaswa kutoka kabla ya uchaguzi mkuu wa Agosti ila kuna mambo hayakuenda sawa, hivyo amewataka mashabiki wakae mkao wa kula kupokea album hiyo ndani ya mwaka huu. Hata hivyo amewataka vijana kujiepusha na  viongozi wanaoeneza siasa za chuki na migawanyiko na badala yake wawe mstari wa mbele kuhubiri amani na mshikamano wakati huu taifa linapoelekea kwenye uchaguzi wa Agosti 9 mwaka huu.

Read More
 BABY MAMA WA MEJJA ASHAMBULIWA MTANDAONI

BABY MAMA WA MEJJA ASHAMBULIWA MTANDAONI

Aliyekuwa mke wa Mejja, Milly Wairimu amejipata pabaya kwenye mitandao ya kijamii baada ya walimwengu kumshambulia kwa madai ya kumvunjia heshima msanii huyo kwenye kumbukizi ya kuzaliwa kwake Mei, 23. Kwenye ujumbe wake aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii Milly Wairimu alimtakia Mejja heri ya siku ya kuzaliwa  na kusindikiza na matusi yakimtakia msanii huyo maisha mabaya kutokana na maovu aliyomtendea kipindi wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi. Sasa ujumbe huo umeonekana kuwakera mashabiki wa Mejja ambao wameshushia kila aina matusi mrembo huyo huku wakimtaka akubali kwamba mahusiano yake na Mejja yalivunja kitambo na badala yake atafute mpenzi wa ndoto yake atakayemliwaza. Utakumbuka mwaka 2021 Milly Wairumu alijitokeza hadharani na kutangaza mtandaoni kwamba waliachana na mejja baada ya msanii huyo kumsaliti kimapenzi.

Read More
 MEJJA ATOA ANGALIZO KWA MASHABIKI ZAKE KUWA MAKINI NA MATAPELI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

MEJJA ATOA ANGALIZO KWA MASHABIKI ZAKE KUWA MAKINI NA MATAPELI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

Msanii nyota nchini Mejja kwa nyingine amewatolea uvivu baadhi ya watu wanaotumia jina lake vibaya kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter. Kupitia  ukurasa wake instagram Mejja amesema akaunti zote ambazo zinatumia jina lake kwenye mtandao wa facebook na twitter ni batili huku akiwataka mashabiki zake wawe waangalifu na matapeli wanaotumia chapa yake kujitakia makuu. Kauli ya Mejja imekuja mara baada ya ukurusa mmoja kwenye mtandao wa twitter unaotumia jina lake kumwagia sifa diamond platinumz jambo ambalo lilipelekea ukurasa rasmi wa lebo ya wcb inayomilikiwa diamond kuchapisha ujumbe huo kwenye mitandao ya kijamii. Hii sio mara ya kwanza kwa mejja kuwaonya watu dhidi ya akaunti feki zinazotumia jina lake kwenye mtandao wa facebook na twitter kwani mwaka wa 2020 alifanya hivyo tena mara  baada ya jamaa mmoja kumtuhumu kuwa alidinda kutokea kwenye interview yake licha ya kumlipa shillingi elfu 12.

Read More
 MEJJA AKANUSHA MADAI YA KURUDIANA NA BABY MAMA WAKE MILLY WAIRIMU

MEJJA AKANUSHA MADAI YA KURUDIANA NA BABY MAMA WAKE MILLY WAIRIMU

Msanii nyota nchini Mejja amekanusha madai yanayotembea kwenye mitandao ya kijamii kuwa amerudiana na baby mama wake Milly Wairimu. Katika mahojiano yake hivi karibuni Mejja amesema madai hayo haya msingi wowote ikizingatiwa kuwa ameyasahau mambo yote yaliyotokea kati yake na mke wake huyo. Kauli ya Mejja inakuja siku chache baada ya Milly Wairimu kudai kuwa Mejja alimtelekeza walipokuwa wanachumbiana. Mrembo huyo alienda mbali zaidi na kuahidi kuaanika kilichopelekea mahusiano yake na mwanamuziki huyo kuingiwa na dosari.

Read More