NYIMBO ZA MICHAEL JACKSON ZAFUTWA KWENYE DIGITAL PLATFORMS ZOTE DUNIANI

NYIMBO ZA MICHAEL JACKSON ZAFUTWA KWENYE DIGITAL PLATFORMS ZOTE DUNIANI

Sony Music ambao ndio wasimamizi wa haki za muziki za marehemu Michael Jackson wameingia kwenye headlines wiki hii. Hii ni baada ya kufuta nyimbo tatu za Michael Jackson kwenye digital platforms zote ikielezwa kuwa nyimbo hizo hakuziimba yeye enzi za uhai wake. Nyimbo hizo ni, “Monster”, “Keep Your Head Up,” na “Breaking News,” ambazo zilikuwa zinapatikana kwenye album ya MJ iitwayo MICHAEL ya mwaka 2010. Album hiyo yenye nyimbo 10 ilitoka mwaka mmoja baada ya Michael Jackson kufariki mwaka wa 2009 Kwa sasa, ni nyimbo saba pekee zimesalia kwenye album hiyo na zinapatikana Spotify, Apple Music, na YouTube   Music.    

Read More