Miley Cyrus Atangaza Ujio wa Albamu Mpya ‘Something Beautiful’
Mwanamuziki nyota Miley Cyrus ametangaza orodha ya nyimbo katika albamu yake ya nane ya studio Something Beautiful, inayotarajiwa kuachiwa rasmi Mei 30 mwaka huu. Albamu hiyo ina jumla ya nyimbo 13, zikiwemo kolabo mbili: “Walk of Fame” akiwa na Brittany Howard, na “Every Girl You’ve Ever Loved” akimshirikisha mwanamitindo Naomi Campbell. Albamu hii imezua msisimko kutokana na mtazamo mpya wa Miley wa kuunganisha muziki na sanaa kutoka nyanja tofauti. Hii inakuja baada ya mafanikio ya Plastic Hearts Album ya Mwaka 2020, na inaashiria hatua nyingine ya ubunifu katika safari yake ya kisanii. Cyrus, ambaye alianza kama nyota wa Hannah Montana, ameendelea kubadilika na kukomaa kisanii, na albamu hii mpya inaonekana kuakisi ukuaji huo. Mashabiki sasa wanasubiri kwa hamu uzinduzi rasmi wa Something Beautiful huku Cyrus akiahidi muziki uliojaa hisia na ubunifu wa hali ya juu.
Read More