MISS CASHY KUMBURUZA MAHAKAMINI KHALIGRAPH JONES KWA KUKWEPA KUTOA MATUNZO KWA MTOTO WAKE

MISS CASHY KUMBURUZA MAHAKAMINI KHALIGRAPH JONES KWA KUKWEPA KUTOA MATUNZO KWA MTOTO WAKE

Mama mtoto wa Khaligraph Jones, Cashy Karimi amefichua kuwa ana mpango kumshtaki rapa huyo baada ya kukataa kutoa matunzo kwa mtoto wao. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Cashy amechapisha picha yake akiwa katika Mahakama ya Milimani na kuandika caption inayosomeka, “Ukiitwa unaitika uilvyo, ukiwa mbali njoo na champali. Ujasiri hutoka kwa Mungu, mwamuzi halisi na mlinzi wa haki. Mungu wa milimani na mabondeni, tangulia mbele yetu.” Ujumbe huo umetafsiriwa na ulimwengu kuwa huenda mrembo huyo amemfungulia mashtaka khaligraph jones kwa hatua ya kukwepa kutoa mahitaji ya msingi kwa mtoto wake. Wawili hao wana mtoto wa kiume pamoja,aitwaye Xolani lakini Cashy amekuwa akishikilia kuwa Khaligraph amekuwa akimtelekeza mtoto wake, huku akiwahudumu watoto wake wengine. Baadhi ya Wakenya kwenye mitandao ya kijamii hata hivyo wamemhimiza Cashy kuendelea na hatua ya kumpigania motto hadi pale khalighraph jones atakaporidhia suala la kutoa matunzo kwa mtoto wao. “Wewe peke yako ndiye unayejua unapitia nini, usiwasikilize watu hawatakuwekea chakula, mvulana anahitaji mambo mengi pigana naye” “Pigana kwa ajili ya mtoto wako wakati wote … Yule yule anayekuambia usishtaki mwanamume au kumburuza mahakamani hatamlisha mwanao” “Usijaribu kupata watoto wakati huwezi kuwatunza …

Read More
 MISS CASHY AANIKA MADHAIFU YA KHALIGRAPH JONES

MISS CASHY AANIKA MADHAIFU YA KHALIGRAPH JONES

Rapa wa kike nchini Miss Cashy amemchana baby daddy Khalighraph Jones kwa mara nyingine kwa madai ya kushindwa kumhudumia mtoto wake. Kupitia mfululizo wa post zake instagram Cashy amekanusha tuhuma zilizoibuwa na walimwengu kwamba anataka kuvunja ndoa ya Papa jones kwa kueleza kuwa mtoto wake alizaliwa miezi kadhaa baada ya khaligraph jones kumpata binti wake wa kwanza. Katika hatua nyingine hitmaker huyo wa ngoma ya “Mi Casa Sucasa” pia ameweka wazi mpango wa kuanza kuzitafuta kampuni ambazo rapa huyo ameingia ubia kufanya naye kazi  ili aweze kupata mgao ambao utamsaidia kutoa mahitaji ya msingi kwa mtoto wao. Hii sio mara ya kwanza Cashy kumsuta vikali Khaligraph Jones kwa madai ya kumtelekeza mtoto wake mwaka wa 2021 alidai rapa huyo alikuwa akitoa visingizo ya kutotoa matunzo kwa mtoto wao kutokana na kanuni za kudhibiti msambao wa corona zilizowekwa na serikali.

Read More
 MISS CASHY AKATA TAMAA KUMSHINIKIZA RAPA KHALIGRAPH JONES KUTOA MATUNZO KWA MTOTO WAO

MISS CASHY AKATA TAMAA KUMSHINIKIZA RAPA KHALIGRAPH JONES KUTOA MATUNZO KWA MTOTO WAO

Female Rapper kutoka Kenya Miss Cashy amedai kuwa licha ya vipimo vya DNA kubaini kuwa rapa Khaligraph Jones ndiye baba wa mtoto wake rap huyo amekataa kutoa matunzo kwa mtoto wake huyo. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni amesema mwaka wa 2021 alifanya vipimo vya DNA baada ya rapa huyo kumshinikiza afanye hivyo ambapo amedai kuwa amelazimika kuhama nairobi kwa ajili ya kumshughulikia mtoto wake huyo. Mrembo huyo amesema hataki tena kuzungumzia suala la Papa Jones kukimbia majukumu ya kumlea mtoto wake kwani amechoka kuonekana anatafuta uhuruma kwa mashabiki wa rapa huyo. Ikumbukwe Miss Cashy amekuwa akimshinikiza Khaligraph Jones  ajukumikie mahitaji ya msingi ya mtoto wao ila rapa huyo amekuwa kimya juu ya swala hilo na hata kukwepa maswali ya waandishi wa habari anapokuwa kwenye mahojiano mbali mbali.

Read More