WILLY PAUL AKIRI KUUMIZWA NA TUHUMA ZA KUMDHALILISHA MISS P KINGONO

WILLY PAUL AKIRI KUUMIZWA NA TUHUMA ZA KUMDHALILISHA MISS P KINGONO

Msanii nyota nchini Willy Paul ameendelea kutoa ushuhuda wa ndani kuhusu maisha yake,amefunguka kwamba alipitia kipindi kigumu mara baada ya kutuhumiwa kumnyanyasa kingono aliyekuwa msanii wake Miss P. Kwenye mahojiano na Munga Eve, Hitmaker huyo wa “Tamu Walahi” amedai kuwa tuhuma hizo ziliathiri afya yake ya akili kiasi cha kupatwa na msongo wa mawazo huku akiri kuwa tangu kipindi hicho hajawahi kurejea katika hali yake ya kawaida kwani amekuwa akiishi kwa hofu. Katika hatua nyingine amesema hatokuja kumsaini msanii yeyote kwenye lebo ya Saldido kwa kuwa wasanii aliowasajili kipindi cha nyuma walimshushia tuhuma za uongo ambazo karibu zimuharibie chapa yake ya muziki. Utakumbuka mwishoni mwa mwaka jana kipindi Miss P anaondoka kwenye lebo ya Saldido alimtuhumu Willy Paul kumdhulumu kijinsia kiasi cha kumlazimisha kutoka nae kimapenzi bila kutumia kinga.

Read More
 MISS P ANYOSHA MAELEZO KUHUSU KUFANYA COLLABO NA WILLY PAUL

MISS P ANYOSHA MAELEZO KUHUSU KUFANYA COLLABO NA WILLY PAUL

Msanii wa kike nchini Miss P amefunguka na kudai kuwa hatawahi fanya collabo tena na msaani mwenzake Willy Paul hadi mwisho wa dunia. Miss P ametujuza hayo kupitia ukurasa wake wa instagram alipomjibu shabiki yake aliyemuomba wafanya kollabo tena na Willy Paul kwa kusema “Naheshimu sana mawazo yako shabiki yangu ila hutokaa uje tena kusikia  kollabo hiyo.” Miss P na Willy P walishawahi kufanya kolabo kupitia nyimbo kama Liar, Fall in Love na Mashallah zilizotoka mwaka wa 2021 lakini walikuja wakaingia kwenye ugomvi mwishoni mwa mwaka jana baada Miss P kujitokeza na kudai kwamba aliondoka kwenye lebo ya muziki ya saldido International kwa sababu alinyanyaswa kimapenzi na willy paul ambaye ndiye mmiliki wa lebo hiyo.

Read More
 ERIC MONDI AFUNGUKA SABABU ZA KUMTEMA MSANII MISS P

ERIC MONDI AFUNGUKA SABABU ZA KUMTEMA MSANII MISS P

Mchekeshaji maarufu nchini Eric Omondi amefunguka sababu za kusitisha kufanya kazi na msanii Miss P baada ya kuchukua jukumu la kumsimamia. Katika mahojiano na mungai Eve,  Omondi amesema changamoto kubwa ambayo kampuni yake ilikutana nayo kutoka kwa Miss P, ni msanii huyo kutoonyesha nia ya kutaka kuzisukuma  kazi zake za muziki  mwenyewe. Mchekeshaji huyo amedai kuwa miss p hakuwa mtu wa kutumia mitandao ya kijamii na mara nyingi ilimbidi asitishe shughuli zake kwa ajili ya kusukuma muziki wa Miss P licha ya kutokuwa mwanamuziki. Eric omondi amesema uzembe wa Miss P kusukuma muziki wake kama msanii ilichangia kampuni yake kuvunja mkataba wa kufanya nae kazi. Kauli ya Eric Omondi imekuja siku chache mara baada ya Miss P kwenye mahojiano na mzazi willy tuva kudai kuwa aliacha kufanya kazi na eric omondi kwa sababu ni mtu haeleweki kwani alipoachia wimbo wake wa “Baby Shower” alikata mawasiliano nae.

Read More