TikToker Mjaka Mfine Atangaza Rasmi Kutafuta Mwanaume Rijali

TikToker Mjaka Mfine Atangaza Rasmi Kutafuta Mwanaume Rijali

TikToker kutoka Kenya, Mjaka Mfine, amekiri kuchoshwa na maisha ya upweke, hatua iliyomfanya kutangaza rasmi kuanza mchakato wa kumtafuta mwanaume rijali atakayempa mapenzi ya dhati. Kupitia video inayotembea mtandaoni, Mrembo huyo amesema yuko tayari kuingia kwenye uhusiano wa kweli na anahitaji mwanaume atakayemhudumia, kumjali na kumuonyesha upendo wa dhati bila maigizo. Ameeleza kuwa kwa sasa anatafuta mapenzi yenye heshima, uaminifu na uthabiti, tofauti na mahusiano ya kuonekana mitandaoni. Mjaka Mfine amesisitiza kuwa anataka mwanaume anayejua wajibu wake, mwenye uwezo wa kusimama kama mwanaume kamili na aliye tayari kumpa usalama wa kihisia pamoja na mapenzi ya kweli. Kauli hiyo imekuja katika kipindi ambacho Mjaka Mfine amekuwa akihusishwa na content creator mwenzake Mokaya, kutokana na ukaribu wao mkubwa ambao umeibua maswali mengi miongoni mwa mashabiki. Hata hivyo, bado haijabainika iwapo ukaribu huo ni wa kikazi au unaashiria uwepo wa uhusiano wa kimapenzi.

Read More
 Mjaka Mfine Akanusha kutoka Kimapenzi na Mokaya

Mjaka Mfine Akanusha kutoka Kimapenzi na Mokaya

Content creator kutoka Kenya Mjaka Mfine amevunja ukimya na kukanusha madai yanayoendelea mtandaoni kwamba ana uhusiano wa kimapenzi na rafiki yake aitwaye Mokaya. Akizungumza katika mahojiano na Shiksha Arora, Mrembo huyo amefafanua kuwa madai hayo hayana msingi na kwamba uhusiano wao uko kwenye misingi ya kazi pekee. Mjaka amesema kuwa yeye na Mokaya wamekuwa wakifanya miradi kadhaa ya pamoja, jambo ambalo limewachochea baadhi ya mashabiki kudhani kwamba wana uhusiano wa karibu zaidi ya kazi. Hata hivyo, amesisitiza kuwa ushirikiano wao umejengwa kwenye taaluma, ubunifu na malengo ya pamoja ya kimaudhui. Utata huo umeibuka kutokana na kemistri inayodhihirika kwenye video zao, hali iliyowafanya baadhi ya wafuasi kufikia hitimisho kwamba wawili hao wana uhusiano wa kimapenzi.

Read More