Mke wa Mkubwa Fella Awajibu Waliomsema Vibaya Mume Wake
Mke wa Mkubwa Fella amejibu vikali watu waliomsema vibaya mume wake wakati alipokuwa akipitia kipindi kigumu cha kiafya. Kupitia instastory yake, mwanamama huyo amechapisha video inayoonyesha yeye na Mkubwa Fella wakifurahia kinywaji, huku hali ya Mkubwa Fella ikionekana kuimarika na kuwa nzuri. Katika video hiyo, wawili hao wameonekana wakiwa na furaha na tabasamu, ishara iliyowafanya wengi kudhani kuwa afya ya Mkubwa Fella inaendelea kuimarika siku hadi siku. Hatua hiyo imetafsiriwa na wengi kama ujumbe mzito kwa wale waliokuwa wakimsema vibaya Mkubwa Fella na hata kumdhihaki kipindi alipokuwa akiomba msaada wa kifedha kutokana na ugonjwa uliomkumba. Ikumbukwe kuwa, baada ya Mke wa Mkubwa Fella kujitokeza hadharani kuomba msaada, baadhi ya watu mitandaoni walimchamba vikali, huku wengine wakifika hatua ya kumtakia mume wake kifo, jambo lililozua hasira na masikitiko makubwa miongoni mwa Watanzania.
Read More