Aliyekuwa mchezaji wa PSG Modeste M’bami afariki dunia
Kiungo wa zamani wa Timu ya Taifa ya Cameroon na klabu ya PSG, Modeste M’bami amefariki siku ya Jumamosi akiwa na umri wa miaka 40 baada ya kupata mshtuko wa moyo PSG imetangaza taarifa hiyo na kutuma salamu za rambirambi za kwa familia yake na walioguswa na msiba huo. “Modeste M’bami ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 40 baada ya kupata mshtuko wa moyo,” ilisema taarifa ya klabu hiyo M’Bami alichezea vilabu kadhaa vya Ufaransa, vikiwemo PSG na Marseille, alishinda Coupe de France akiwa na klabu ya PSG mwaka wa 2004 na 2006 Alifunga mabao matatu katika mechi 37 alizoichezea Cameroon na alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshinda dhahabu kwenye Michezo ya Olimpiki ya Sydney mwaka wa 2000 nchini Australia M’bami pia alikuwa sehemu ya timu ya Cameroon iliyocheza fainali ya Kombe la Shirikisho la FIFA la 2003 Kiungo huyo alicheza katika nchini kadhaa kama vile Hispania, China na Saudi Arabia kabla ya kustaafu mnamo 2016, akichagua kusalia katika, Normandy nchini Ufaransa baada ya kustaafu.
Read More