MONI CENTROZONE ATHIBITISHA KOLABO YAKE  NA MSANII WA KONDE GANG, ANJELLA

MONI CENTROZONE ATHIBITISHA KOLABO YAKE NA MSANII WA KONDE GANG, ANJELLA

Female singer kutoka lebo ya Konde Gang Worldwide, msanii Anjella huenda tukamsikia kwenye ngoma ijayo ya rapa Moni Centrozone. Rapa huyo mzaliwa wa Majengo Sokoni, Dodoma kupitia ukurasa wake wa Instagram ame-share picha akiwa na Anjella na kueleza kwamba angetamani mrembo huyo asikike kwenye moja ya ngoma yake, ikiwa ni kolabo yake ya kwanza na msanii wa kike. “Queen anjella Watu wa Majengo itabidi utuchapie kibwagizo kwenye mdundo mmoja wa HipHop. Itakuwa collabo yangu ya kwanza na msanii wa kike”. Aliandika Moni kwenye Instagram page yake. Sanjari na hilo, wawili hao Jumamosi hii iliyopita walishusha burudani kwenye jukwaa la tamasha la Harmonize, Afro East Carnival, jijini Dar es salaam.

Read More
 RAPPER MONI CENTROZONE AWABARIKI MASHABIKI NA ROAD TO MAZENGO EP

RAPPER MONI CENTROZONE AWABARIKI MASHABIKI NA ROAD TO MAZENGO EP

Msanii wa Hip Hop kutoka tanzania, Moni Centrozone ameachia rasmi Extended Playlist (EP) yake mpya inayokwenda kwa jina la Road To Mazengo. EP hiyo ina nyimbo tano alizowashirikisha wasanii watano ambao ni Young Lunya, Slimsal, One Six na wengine wengi. Maproduza waliohusika kutayarisha EP hiyo ni S2kizzy, Trakks, Slimsal, Pol Maker na Tony Drizy. Utakumbuka EP hiyo ambayo ni ya kwanza kwa Moni Centrozone inatoka chini lebo ya muziki ya RoofTop Entertainment.

Read More