YKEE BENDA ATAKA SERIKALI YA UGANDA KUTENGA SIKU YA KITAIFA KUMKUMBUKA MAREHEMU MOZEY RADIO

YKEE BENDA ATAKA SERIKALI YA UGANDA KUTENGA SIKU YA KITAIFA KUMKUMBUKA MAREHEMU MOZEY RADIO

Bosi wa lebo ya muziki ya Mpaka Records msanii Ykee Benda ameitaka serikali ya Uganda kuiweka Februari mosi ya kila mwaka kuwa Sikikuu ya Kitaifa kumkumbuka Marehemu Mozey Radio ambaye alifariki tarehe hiyo mwaka wa 2018. Akizungumza huko Kagga nchini Uganda ambako Mozey Radio alipumzishwa mwaka wa 2018, Ykee Benda amesema mwendazake mozey Radio alikuwa nguzo muhimu katika taifa la uganda, hivyo ni vigumu kujaza pengo aliloliacha kwenye tasnia ya muziki nchini humo. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Obangaina” ameenda mbali zaidi na kusema kuwa kipindi anachipukia kwenye tasnia ya muziki nchini uganda alikuwa na mazoea ya kuiba mashairi ya nyimbo za mozey Radio na kuyatumia kwenye nyimbo zake.

Read More
 WEASEL MANIZZO MBIONI KUJA NA TAMASHA LA KILA MWAKA KUMUENZI MWENDAZAKE MOZEY RADIO

WEASEL MANIZZO MBIONI KUJA NA TAMASHA LA KILA MWAKA KUMUENZI MWENDAZAKE MOZEY RADIO

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Weasel Manizo ameweka wazi mpango wa kuja na tamasha la kila mwaka kwa ajili ya kumpa heshima marehemu Mozey Radio. Msanii huyo ambaye alikuwa mwanakikundi wa Goodlyfe Entertainment, amesema tamasha hilo litaitwa Radio Festival na litaanza mapema mwaka wa 2022. Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wamemjia juu baada ya msanii huyo kususia kuhudhuria maombi ya kumkumbuka marehemu Radio wiki iliyopita wakimtaja kuwa mnafiki kwa kushindwa kuendeleza nyayo za mozey radio kwenye tasnia ya muziki nchini  Uganda. Duru za kuaminika zinasema Weasel Manizo alisusia maombi kutokana na tofauti walizonazo na Familia ya Mozey Radio kuhusu mirabaha ya muziki wa Radio. Utakumbuka Mozey Radio ambaye alikuwa anaunda kundi la Goodlyfe alifariki mwezi Februari mwaka wa 2018 baada ya kuingia kwenye ugomvi na mlinzi wa night club moja huko Kampala uganda.

Read More