LAVA LAVA ATANGAZA UJIO MPYA,OKTOBA 23

LAVA LAVA ATANGAZA UJIO MPYA,OKTOBA 23

Msanii wa bongofleva kutoka WCB, Lava Lava ametangaza kuja na project mpya, Oktoba 23, mwaka wa 2021. Lava Lava ambaye hivi karibuni amefuta picha zake zote kwenye ukurasa wake wa Instagram, amechapicha ujumbe kuhashiria Oktoba 23, mwaka huu atakuwa na kitu. Ikumbukwe mwimbaji huyo ambaye mwaka huu ameachia  EP iitwayo ‘Promise’, tayari alitangaza kukamilika kwa albamu yake. Mwaka huu wasanii wa WCB kama Rayvanny na Mbosso wameweza kutoa albamu zao na zinazidi kufanya vizuri.

Read More
 SAUTI SOL MBIONI KUJA NA ALBUM MPYA

SAUTI SOL MBIONI KUJA NA ALBUM MPYA

Kundi la muziki nchini sauti sol wametangaza mwezi ambao wataichia album yao ya sita tangu waanze safari yao ya muziki. Kupitia barua ya wazi waliyoishare kwenye ukurasa wao wa instagram sauti sol wamesema album yao mpya itaingia sokoni mwezi mei mwaka wa 2022. Wakali hao wa ngoma ya Suzzana wamesema kabla ya kuachia album yao mpya, wataachia singo yao mpya mwezi Disemba mwaka huu ambapo wamesema kwamba wataweka wazi tarehe ambayo wataachia project hiyo. Sanjari na hilo wametusanua kwamba wanakuja na documentary yao iitwayo Alone Together ambayo itazungumzia changomoto ambazo wasanii wa kundi la sauti sol wamepitia tangu ujio wa janga la korona. Kauli ya sauti sol inakuja mara baada ya kufanikisha tamasha lao la kimuziki liitwalo UK residency lilofanyika nchini uingereza mapema mwezi huu.

Read More