Mr. Blue Asema Sifa Zilimpoteza Kwenye Muziki, Ajuta Kuwadharau Watu

Mr. Blue Asema Sifa Zilimpoteza Kwenye Muziki, Ajuta Kuwadharau Watu

Rapa kutoka Tanzania Mr. Blue amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu changamoto zilizomfanya apotee kwenye muziki, akisema sifa na majivuno vilimchanganya na kumfanya awadharau watu waliokuwa sehemu ya mafanikio yake. Kwenye mkao na waandishi wa habari, Blue amesema kuwa kipindi anaanza kupata umaarufu, alijikuta akibadilika tabia na kuanza kujiona amefika, hali iliyomfanya asipokee simu, asiwasalimie watu, na kuwakosea heshima waliokuwa wakimuunga mkono katika safari yake ya muziki. Mr. Blue anasema hatua hiyo ilimrudisha nyuma kwa kiasi kikubwa, kwani alijikuta akikosa marafiki, ushirikiano, na hata mashabiki waliokuwa wakimuamini. Ameeleza kuwa majivuno hayo yalimnyima fursa ya kuendelea kukua kimuziki, jambo analoliona sasa kama funzo kubwa maishani. Kwa sasa, msanii huyo amesema anajutia sana tabia hiyo na kukiri kwamba majivuno hayamjengi msanii bali humuangusha. Anasema amejifunza umuhimu wa unyenyekevu na anatamani Mungu ampe nafasi nyingine ya kurejea kwenye umaarufu akiwa na mtazamo mpya.

Read More