Mr. T aonya wasanii dhidi ya kiki, Adai inaharibu soko la muziki

Mr. T aonya wasanii dhidi ya kiki, Adai inaharibu soko la muziki

Baada ya wasanii kibao kutengeneza kiki kwa ajili kukamata attention ya mashabiki wao juu ya ujio wa kazi zao, Mwimbaji aliyegeukia ukasisi Mr. T yeye anapingana na kitendo hicho kwa kusema kwamba soko la muziki linakufa kwa njia hiyo. Mr. T amefunguka na kusema kitendo cha wasanii kutengeneza kiki ili waweze kuzungumziwa katika media kuliko kazi zao inaua na kuwaharibu mashabiki kutokana na kufuatilia sana skendo za mastaa kuliko kazi zao. Akizungumza na podcast ya Presenter Ali amesema kuwa kitendo hicho kimewaharibu wasanii wachanga ambao wanataka kutoka na kufikiria kuachia kiki kwanza ili wajulikane kwa haraka na kazi zao kuweza kufika mbali. Hata hivyo amesisitiza kuwa ingawa kiki ina mchango kwenye muziki ila zifanyike kwa ustaarabu kwani inaweza kuwa shubiri pale wasanii wanapotupiana maneno machafu mtandaoni.

Read More
 MR T AKIRI KUMUOMBA MSAMAHA MSANII WA NYIMBO ZA INJILI ROSE MUHANDO BAADA YA KUMVUNJIA HESHIMA 2021

MR T AKIRI KUMUOMBA MSAMAHA MSANII WA NYIMBO ZA INJILI ROSE MUHANDO BAADA YA KUMVUNJIA HESHIMA 2021

Mwanamuziki wa injili aliyegeukia ukasisi kutoka nchini Kenya Mr. T amekiri kumuomba msamaha msanii wa nyimbo za injili nchini Tanzania Rose Muhando baada ya kumvunjia heshima mwaka wa 2021. Kwenye mahojiano na mpasho Mr. T  amesema alichukua maamuzi hayo baada ya watu kumshambulia kwenye mitandao ya kijamii ambapo amedai kwamba hakuwa na nia ya kumharibia jina Rose Muhando ila alikuwa anatoa mfano kwa wakristo. Hitmaker huyo wa ngoma ya Finje Finje amesema hana ugomvi wowote na  Rose Muhando akizingatiwa kuwa amekuwa akimtakia mema kwenye harakati za kuupeleka muziki wake kwenye hatua nyingine. Mr. T aligonga vichwa vya habari nchini Kenya mara baada ya kumtolea uvivu Rose Muhando kwenye moja ya ibada yake ya kanisani kwa kusema kwamba anguko la Rose Muhando kimuziki lilikuja kufuatia hatua yake kujiunga na lebo ya muziki Sony Music. Hata hivyo mashabiki wengi wa muziki wa injili Afrika Mashariki  hawakufurahishwa na matamashi ya Mr. T jambo ambalo lilimlazimu Rose Muhando kujitokeza na kumsuta  vikali kasisi huyo kwa kumharibia chapa yake ya muziki ambayo ameitengeneza kwa miaka nyingi.      

Read More