Utunzi wa nyimbo haulipi – Mudra

Utunzi wa nyimbo haulipi – Mudra

Hitmaker wa “Balo Balo”, Msanii Mudra amefunguka sababu za kuachana na masuala ya utunzi wa nyimbo. Mudra amesema kipindi cha nyuma alikuwa anawaandikia nyimbo baadhi ya wasanii nchini Uganda akiwemo Cindy Sanyu na Karole Kasita lakini uandishi wa nyimbo kwa upande wake haulipi. Aidha amesema wasanii wanaoandikiwa nyimbo ndio ufaidi pakubwa huku waandishi wakibaki kwenye lindi la umasiki. Hata hivyo amesema atawaandikia wasanii wengine nyimbo akiwa hana shughuli ya kufanya ila kwa sasa ameelekeza nguvu zake kwenye suala la kuboresha kazi zake za muziki kwani ndio njia pekee itakayoboresha maisha yake. Mudra amekuwa kwenye tasnia ya muziki kwa kipindi kirefu lakini watu walikuja kumfahamu alipoachia hit single yake “Muyayu”, ambayo ilisumbua sana kwenye chati mbali mbali za muziki.

Read More