ANGELINA ATANGAZA KUACHA MUZIKI

ANGELINA ATANGAZA KUACHA MUZIKI

Nyota wa muziki nchini uganda Angelina amedokeza mpango wa kuachana kabisa na masuala ya muziki. Angelina ameweka wazi hayo kupitia ukurasa wake wa twitter ambapo amesema ataacha muziki mwaka wa 2022 baada ya kuachia project yake ya mwisho ambayo amekuwa akiifanyia kazi kwa muda. Kulingana na mrembo huyo baada ya kuacha muziki ataelekeza nguvu zake kwingine katika suala zima la kujitafutia riziki. Hata hivyo tweet yake hiyo haikukaa kwa muda kwenye ukurasa wake twitter kwani alikuja akaifuta baada ya kuchapisha. Angelina amekuwa kwenye kiwanda cha muziki nchini Uganda kwa muda wa miaka kumi na ametoa hits kali kama Go Down, Ghetto Lovin, Ronaldo na nyingine kibao.

Read More
 B CLASSIC AACHIA KAZI YAKE YA MWISHO

B CLASSIC AACHIA KAZI YAKE YA MWISHO

Msanii wa muziki nchini Kenya, Dennis Manja maarufu kama B Classic ameachia wimbo wake wa mwisho baada ya kutangaza nia yake ya kutaka kuacha muziki.   B Classic alidai kuwa anaacha muziki na kugeukia kazi ya ufundi wa magari baada ya kutoridhishwa na mapokezi ya kazi zake pindi anapoachia muziki mpya.   B Classic mkali wa wimbo wa Pisi Kali uliofanya vizuri mapema mwezi Agosti mwaka huu, ameachia  ‘Utawezana Kweli’, wimbo anaodai kuwa itakuwa kazi yake ya mwisho.   Wimbo huo umetayarishwa na Prodyuza Denzel huku video ikaongozwa na Director Rahim chini ya lebo ya muziki ya Champions Studio yenye makao yake jijini Nairobi.            

Read More