Otile Brown Aumizwa na Habari za Ndoa ya Nabayet, Aandika Ujumbe wa Hisia Kali

Otile Brown Aumizwa na Habari za Ndoa ya Nabayet, Aandika Ujumbe wa Hisia Kali

Mwanamuziki wa Bongo R&B kutoka Kenya, Otile Brown, ameibua hisia mtandaoni baada ya kuonyesha maumivu na mshangao kufuatia habari za aliyekuwa mpenzi wake, Nabayet kutoka Ethiopia, kufunga ndoa. Kupitia Insta Story yake, Otile alionekana kushindwa kuficha hisia zake, hasa kwa kuwa alimtaja Nabayet katika wimbo wake mpya unaotarajiwa kuachiwa. Ameandika:  “How does she go & get married after mentioning her on my new song dropping tomorrow… now I feel dueh…”,  Otile aliandika hisia nyingi Maneno hayo yameibua hisia mseto mitandaoni, huku mashabiki wake wakimfariji na wengine wakihisi kwamba bado ana hisia kwa mrembo huyo. Uhusiano wa Otile Brown na Nabayet ulikuwa wa muda mrefu na wa hadharani, uliovutia mashabiki wengi kutoka Afrika Mashariki na Ethiopia. Wawili hao walionekana kuwa na mahusiano yenye upendo mkubwa kabla ya kuachana kimya kimya miaka michache iliyopita. Kabla ya habari za ndoa ya Nabayet, Otile alikuwa ameonekana kuendelea na maisha, lakini ujumbe huu mpya unaonyesha pengine bado kuna hisia zilizobaki. Mashabiki sasa wanasubiri kwa hamu wimbo mpya wa Otile Brown ili kusikia alivyomzungumzia Nabayet, huku wengi wakijiuliza kama hii itaathiri maudhui au hisia za kazi hiyo.

Read More
 Nabayet, Mpenzi wa Zamani wa Otile Brown, Afunga Ndoa Kwenye Harusi ya Kifahari Ethiopia

Nabayet, Mpenzi wa Zamani wa Otile Brown, Afunga Ndoa Kwenye Harusi ya Kifahari Ethiopia

Mwanamitindo maarufu kutoka Ethiopia,Nabayet, ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa msanii nyota wa Kenya Otile Brown, ameaga rasmi maisha ya u-single baada ya kufunga ndoa kwenye harusi ya kifahari iliyofanyika nchini mwake mwishoni mwa wiki. Harusi hiyo, iliyohudhuriwa na familia, marafiki wa karibu na watu mashuhuri kutoka sekta ya mitindo na burudani, ilifanyika katika hoteli ya kifahari jijini Addis Ababa. Nabayet alionekana mrembo kupindukia akiwa amevalia gauni jeupe la harusi lililobuniwa na mbunifu maarufu wa mitindo wa Ethiopia. Video na picha za tukio hilo zimeenea kwenye mitandao ya kijamii, huku mashabiki wakimpongeza kwa hatua hiyo mpya katika maisha yake. Ingawa hakufichua jina la mchumba wake, mashabiki walionekana kushangilia penzi jipya la mrembo huyo ambaye amekuwa akipunguza sana kuweka maisha yake ya kimapenzi hadharani. Nabayet aliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na Otile Brown mwaka 2019, na wawili hao walivutia mashabiki wengi kwa mahusiano yao ya kuvutia yaliyokuwa yakisambazwa kupitia mitandao ya kijamii. Hata hivyo, uhusiano huo uliisha baada ya muda kutokana na tofauti zao za kimtazamo. Otile Brown bado hajatoa kauli rasmi kuhusu harusi hiyo ya mpenzi wake wa zamani. Mashabiki wa Nabayet wameendelea kumpongeza kwa hatua hiyo kubwa, wakimtakia heri katika maisha mapya ya ndoa.

Read More
 Otile Brown afunguka kuhusu kujipendekeza kwa mpenzi wake wa zamani Nabayet

Otile Brown afunguka kuhusu kujipendekeza kwa mpenzi wake wa zamani Nabayet

Staa wa muziki nchini Otile Brown amewajibu wanaodai kuwa anajipendekeza kwa mpenzi wake wa zamani Nabayet licha ya mahusiano yao kuvunjika. Otile ambaye amerejea nchini baada ya kukamilisha ziara ya miezi miwili nchini marekani amewashangaa wanaomsema vibaya kuwa bado anamzimia kimapenzi mrembo huyo kwa kusema kuwa hajutii kitendo cha kumtumia salamu za heri kwenye kumbukizi ya kuzaliwa kwake kwani ni moja kati ya watu ambao anawapenda sana. Otile Brown na Nabayet walikuwa kwenye mahusiano kwa kipindi cha miaka miwili lakini mahusiano yalikuja kuvunjika mwaka wa 2020 kutokana na umbali kati yao. Utakumbuka mwaka wa 2019 Otile Brown aliachia wimbo wa kusifia urembo wa Nabayet baada ya penzi lao kunoga.

Read More
 OTILE BROWN ATHIBITISHA KUACHANA NA MPENZI WAKE WA SIKU NYINGI NABAYET

OTILE BROWN ATHIBITISHA KUACHANA NA MPENZI WAKE WA SIKU NYINGI NABAYET

Staa wa muziki nchini Otile Brown, ametangaza kuachana na Mpenzi wake raia wa Ethiopia Nabayet baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa muda wa miaka mitatu. Kupitia ukurasa wake wa instagram  Otile Brown amesema amechukua maamuzi ya kuachana na mpenzi wake huyo baada ya kuafikia makubaliano ya pamoja ambapo amedai kuwa wataendelea kuwa marafiki. Hata hivyo chanzo cha wawili hao kuachana hajaweka wazi ila sio mara ya kwanza kufanya hivyo kwani kipindi cha nyuma wamekuwa na mazoea ya kuachana na kisha mwisho wa siku wanarudiana Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wamehoji huenda Otile Brown anatengeza  mazingira ya kumzinguziwa kabla ya ujio wa ngoma yake mpya Ikumbukwe kuwa penzi la Otile Brown na Nabayet lilianza rasmi mwishoni mwa mwaka 2018  miezi kadhaa baada ya kuachana na aliyekua mpenzi wake Verah Sidika.

Read More