NACADA Yajibu Bien: “Sio Unafiki Bali Ni Hatua ya Kulinda Afya ya Umma”
Mamlaka ya Kitaifa ya Kudhibiti Matumizi ya Dawa za Kulevya (NACADA) imejibu vikali matamshi ya msanii Bien wa kundi la Sauti Sol, aliyekosoa pendekezo la kuwapiga marufuku wasanii na watu mashuhuri kutangaza bidhaa za vileo. Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, NACADA imesisitiza kuwa hatua hiyo haifungamani na unafiki wa maadili wala juhudi za kukandamiza uhuru wa wasanii, bali inalenga kulinda afya ya umma hasa vijana, ambao ndio walio katika hatari zaidi ya kushawishika na ulevi kupitia ushawishi wa watu maarufu. Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Bien kusema kuwa hatua hiyo ni unafiki na kwamba wasanii wana haki ya kujipatia kipato kupitia matangazo ya kibiashara. Hata hivyo, NACADA imetoa wito kwa wasanii kutumia ushawishi wao kuhamasisha maisha yenye afya na kutoa matumaini kwa jamii badala ya kushabikia bidhaa zinazoweza kuwa hatari kwa maisha ya wengi.
Read More