Nadia Mukami Afichua Anatarajia Mtoto Mwingine na Arrow Bwoy
Mwanamuziki nyota wa Kenya, Nadia Mukami, amefichua kuwa anatarajia mtoto wa pili na mpenzi wake ambaye pia ni msanii maarufu, Arrow Bwoy. Kupitia ujumbe wa hisia aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii, Nadia alisema anajisikia kubarikiwa mno, huku akieleza namna ujio wa mtoto wao wa kwanza ulivyobadili maisha yake kwa njia chanya. “Naamini watoto huja na baraka zao. Mtoto wangu wa kwanza alikuja na sahani, lakini huyu wa pili amekuja na sahani kubwa zaidi,” alisema Nadia kwa furaha. Taarifa hiyo limepokelewa kwa furaha na mashabiki wao, wengi wakituma salamu za pongezi huku wengine wakimsifu Nadia kwa kuwa mfano wa mama kijana mwenye maono na nidhamu ya kazi. Nadia na Arrow Bwoy walipata mtoto wao wa kwanza mwaka wa 2022, na wamekuwa wakionesha maisha yao ya kifamilia hadharani huku wakidumisha mapenzi yao jukwaani na nje ya jukwaa. Wapenzi hao wameendelea kushirikiana katika muziki, biashara, na malezi, na sasa wanaonekana kuimarika zaidi kama familia.
Read More