NAHREEL WA NAVY KENZO AKANUSHA MADAI YA KUPOKONYWA NYOTA YAO NA DIAMOND PLATNUMZ

NAHREEL WA NAVY KENZO AKANUSHA MADAI YA KUPOKONYWA NYOTA YAO NA DIAMOND PLATNUMZ

Msanii na Prodyuza, Nahreel kutoka kundi la Navy Kenzo amesema sio kweli kwamba Diamond Platnumz anachukua nyota za wasanii mwenzake kupitia kolabo bali ni mipango ya wasanii wenyewe. Akizungumza hilo, Nahreel amesema mashabiki huwa wanaongea vitu vingi na ni haki yao kwa sababu wanahitaji huduma yao mara kwa mara, wanapokaa kimya wanaona kama wamepotea au kuchukuliwa nyota lakini sio kweli. “Hayo mambo ya kuchukuliana nyota sio kweli, sisi tunapitia changamoto nyingi, hata ambao wanawaona sehemu nzuri juu hata wenyewe pengine kuna changamoto wanapitia” amesema Nahreel. Nahreel amesema wanapenda kufanya kazi kwa mipango kwa sababu wanaweka nguvu nyingi kwenye ubunifu na namna ya kuandaa muziki na video, hivyo wanatakiwa kuwa watulivu katika kuandaa kitu kizuri. “Mambo ya nyota hapana, tumekaa kimya kwa sababu ya vitu vingi, sio muziki tu, tuna Academy ya mpira, Aika ana biashara zake, kwa hiyo tumekuwa tukiweka nguvu huku ili mambo yaende, baadaye muda mzuri ukifika tunaweka tena nguvu kwenye muziki,” amesema. Hata hivyo amesema wao kama Navy Kenzo wamekuwa wakifanya muziki kwa muda mrefu, hivyo ni vigumu kusema watakuwa wanafanya tu muziki, lazima wewe wanajihusisha na vitu vingine. Utakumbuka Septemba 28, mwaka wa 2018 Navy Kenzo waliachia video ya wimbo wao, Katika waliomshirikisha Diamond, hadi sasa video yake katika mtandao wa YouTube imepata views milioni 26.1 na kuwa video yao pekee iliyotazamwa zaidi. Lakini tangu wakati huo hakuna video yoyote waliyotoa Navy Kenzo iliyofanikiwa kufikisha walau views milioni 1 licha ya kuachia ngoma kali kama Roll It, Magical, Why Now, Bampa 2 Bampa, Only One na Nisogelee.

Read More
 NAHREEL AJIBU KUPOTEZWA NA KOLABO YA DIAMOND

NAHREEL AJIBU KUPOTEZWA NA KOLABO YA DIAMOND

Kundi la muziki kutoka Tanzania, Navy Kenzo limeonyesha kupuuzia madai kuwa wamepotea tangu kuachia kolabo yao na Diamond Platnumz, kupitia wimbo uitwao “Katika”. Memba wa kundi hilo, msanii Nahreel amepangua kauli hiyo kutoka kwa shabiki mmoja ambaye aliacha komenti kwenye ukurasa wa instagram wa Nahreel, kwa kuandika; “Diamond mbaya sana toka mfanye naye wimbo dah, hamsikiki naumia sana”, Nahreel alimjibu shabiki huyo kwa kumuandikia; “Kaa mkao wa kula”. “Katika” ni kolabo iliyowakutanisha Navy Kenzo na Diamond Platnumz, ilitoka mwaka 2018. Ikumbukwe Navy Kenzo kwa sasa wanajiandaa kuachia album yao ya nne baada ya kuachia Hold Me Back ya mwaka 2015, AIM – Above Inna Minute ya mwaka wa 2017 na Story Of The African Mob ya mwaka 2020.

Read More
 PRODYUZA WA BONGOFLEVA NAHREEL AKANUSHA KUWA NA MTOTO NJE YA NDOA

PRODYUZA WA BONGOFLEVA NAHREEL AKANUSHA KUWA NA MTOTO NJE YA NDOA

Msanii wa muziki Bongofleva Nahreel amekanusha vikali taarifa za kuzaa nje ya mahusiano yake na mpenzi wake, Aika ambaye wanaunda wote kundi la Navy Kenzo. Nahreel kupitia ukurasa wake wa Instagram ametaka wote wanaosambaza taarifa hizo kuiheshimu familia yake ambapo amesisitiza ana watoto wawili tu aliojaliwa na Aika. “Kutokana na habari zinazosambaa kwenye blog mbalimbali na watu mbalimbali maarufu pia wamekuwa wakipost bila kuwa na ushahidi wowote, hizi habari sio za kweli. “Nina watoto wawili, Gold na Jamaika, na nimezaa na mwanamke mmojaAika, kuweni makini mnapotoa habari familia yetu haiendekezi Umbeya ila hii imevuka mipaka.” Ameandika Nahreel kupitia Instagram page yake. Utakumbuka Nahreel na Aika wako mbioni kuachia album yao mpya inayokwenda kwa jina la Dread & Love ambayo wamedai imekamilika kwa asilimia 70.

Read More