NASHA TRAVIS AKIRI KIKI INA MCHANGO MKUBWA KWA WASANII

NASHA TRAVIS AKIRI KIKI INA MCHANGO MKUBWA KWA WASANII

Msanii Nasha Travis amedai kuwa kiki zinaweza kuwa na mchango fulani katika muziki wa msanii tofauti na watu wengi ambao hupinga suala hilo. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Nasha amesema anaona ni sawa tu kwa wasanii kutengeneza matukio ili wazungumziwe mtandaoni kwani inasaidia kwa kiasi kikubwa kuinua muziki wao. Katika hatua nyingine Mrembo huyo ambaye anafanya vizuri na single yake mpya “Naiwe” amesisitiza kuwa ingawa kiki ina mchango kwenye muziki, inapaswa kufanywa kwa ustaarabu kwani inaweza kuwa shubiri pale wasanii wanapotupiana maneno machafu mtandaoni.

Read More
 NASHA TRAVIS ADAI ATOA RAI KWA WASANII WA KENYA KUPUNGUZA KIKI

NASHA TRAVIS ADAI ATOA RAI KWA WASANII WA KENYA KUPUNGUZA KIKI

Msanii wa kike nchini Nasha Travis amewaomba wasanii wa Kenya kupunguza kiki na kuongeza bidii katika muziki. Katika mahojiano na podcast ya Nicholas Kioko kwenye mtandao wa Youtube, Nasha Travis amewataka wasanii nchini wazingatie suala la kutayarisha muziki mzuri badala ya kiki ambazo hazina msingi wowote. Kulingana na Nasha, muziki ni kama bidhaa na mashabiki hutumia bidhaa hiyo kulingana na ubora wake. Mrembo huyo kutoka Bar Nelson Empire amesema anatamani sana kuona wasanii wa Kenya wanajihusisha na muziki pekee na wala si masuala mengine ya kuwapa umaarufu mtandaoni. Ikumbukwe kwa sasa Nasha Travis anafanya vizuri na EP yake mpya African Sound Queen ambayo iliingia sokoni Aprili mosi mwaka huu ikiwa na mikwaju 7 za moto.

Read More
 NASHA TRAVIS AACHIA RASMI THE AFRICAN SOUND QUEEN EP

NASHA TRAVIS AACHIA RASMI THE AFRICAN SOUND QUEEN EP

Msanii kike nchini Nasha Travis ameachia rasmi EP yake mpya inayokwenda kwa jina la  The African Sound Queen Ep   . The African Sound Queen Ep ina jumla ya ngoma 6 za moto na bonus track moja ambazo  zimetayarishwa na maprodyuza kama  Kashkeed, Alexis on the beat, Bonga pamoja na Mumo beats. Lakini pia mrembo huyo amewashirikisha wakali kama Madini Classic, Joefes, Japesa, Bonga de Alpha na DJ Lyta. The African Sound Queen Ep ni Kazi ya kwanza kwa mtu mzima Nasha Travis tangu aanze safari yake ya muziki na inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mtandao wa kukisikiliza na kupakua muziki wa Boomplay Kenya.

Read More