Navy Kenzo watajwa kushirikishwa kwenye album ya Kampuni ya EMPIRE

Navy Kenzo watajwa kushirikishwa kwenye album ya Kampuni ya EMPIRE

Kundi la muziki maarufu kutoka nchini Tanzania Navy Kenzo wametajwa kuwa ni moja wapo ya wasanii watakao unda tracklist ya album iliyoandaliwa na Kampuni ya usambazaji wa muziki ya EMPIRE iliyopo San Francisco, Marekani. Taarifa hiyo ambayo imethibitishwa na ukurasa rasmi wa instagram wa Empire Africa pia ikiandikwa kwenye tovuti kubwa kama Billboard, Hot97 na Variety za nchini marekani, album hiyo inatajwa kuwa na mjumuisho wa mastaa wa muziki kutoka Afrika wakiwemo Olamide, Fireboy DML, Kizz Daniel, Buju BNXN, Asake, Black Sherif na wengineo wengi. Album hiyo imepewa jina la “Where we come from” na inatarajiwa kutoka mwezi ujao, Novemba 18, 2022. Utakumbuka Empire Africa wameamua kuja na album hii baada ya muziki kutoka barani Afrika kusikilizwa na kupendwa kwa kiwango kikubwa Duniani.

Read More
 NAHREEL WA NAVY KENZO AKANUSHA MADAI YA KUPOKONYWA NYOTA YAO NA DIAMOND PLATNUMZ

NAHREEL WA NAVY KENZO AKANUSHA MADAI YA KUPOKONYWA NYOTA YAO NA DIAMOND PLATNUMZ

Msanii na Prodyuza, Nahreel kutoka kundi la Navy Kenzo amesema sio kweli kwamba Diamond Platnumz anachukua nyota za wasanii mwenzake kupitia kolabo bali ni mipango ya wasanii wenyewe. Akizungumza hilo, Nahreel amesema mashabiki huwa wanaongea vitu vingi na ni haki yao kwa sababu wanahitaji huduma yao mara kwa mara, wanapokaa kimya wanaona kama wamepotea au kuchukuliwa nyota lakini sio kweli. “Hayo mambo ya kuchukuliana nyota sio kweli, sisi tunapitia changamoto nyingi, hata ambao wanawaona sehemu nzuri juu hata wenyewe pengine kuna changamoto wanapitia” amesema Nahreel. Nahreel amesema wanapenda kufanya kazi kwa mipango kwa sababu wanaweka nguvu nyingi kwenye ubunifu na namna ya kuandaa muziki na video, hivyo wanatakiwa kuwa watulivu katika kuandaa kitu kizuri. “Mambo ya nyota hapana, tumekaa kimya kwa sababu ya vitu vingi, sio muziki tu, tuna Academy ya mpira, Aika ana biashara zake, kwa hiyo tumekuwa tukiweka nguvu huku ili mambo yaende, baadaye muda mzuri ukifika tunaweka tena nguvu kwenye muziki,” amesema. Hata hivyo amesema wao kama Navy Kenzo wamekuwa wakifanya muziki kwa muda mrefu, hivyo ni vigumu kusema watakuwa wanafanya tu muziki, lazima wewe wanajihusisha na vitu vingine. Utakumbuka Septemba 28, mwaka wa 2018 Navy Kenzo waliachia video ya wimbo wao, Katika waliomshirikisha Diamond, hadi sasa video yake katika mtandao wa YouTube imepata views milioni 26.1 na kuwa video yao pekee iliyotazamwa zaidi. Lakini tangu wakati huo hakuna video yoyote waliyotoa Navy Kenzo iliyofanikiwa kufikisha walau views milioni 1 licha ya kuachia ngoma kali kama Roll It, Magical, Why Now, Bampa 2 Bampa, Only One na Nisogelee.

Read More
 NAHREEL AJIBU KUPOTEZWA NA KOLABO YA DIAMOND

NAHREEL AJIBU KUPOTEZWA NA KOLABO YA DIAMOND

Kundi la muziki kutoka Tanzania, Navy Kenzo limeonyesha kupuuzia madai kuwa wamepotea tangu kuachia kolabo yao na Diamond Platnumz, kupitia wimbo uitwao “Katika”. Memba wa kundi hilo, msanii Nahreel amepangua kauli hiyo kutoka kwa shabiki mmoja ambaye aliacha komenti kwenye ukurasa wa instagram wa Nahreel, kwa kuandika; “Diamond mbaya sana toka mfanye naye wimbo dah, hamsikiki naumia sana”, Nahreel alimjibu shabiki huyo kwa kumuandikia; “Kaa mkao wa kula”. “Katika” ni kolabo iliyowakutanisha Navy Kenzo na Diamond Platnumz, ilitoka mwaka 2018. Ikumbukwe Navy Kenzo kwa sasa wanajiandaa kuachia album yao ya nne baada ya kuachia Hold Me Back ya mwaka 2015, AIM – Above Inna Minute ya mwaka wa 2017 na Story Of The African Mob ya mwaka 2020.

Read More
 ALBUM MPYA YA NAVY KENZO “DREAD & LOVE” YAKAMILIKA KWA ASILIMIA 70

ALBUM MPYA YA NAVY KENZO “DREAD & LOVE” YAKAMILIKA KWA ASILIMIA 70

Kundi la muziki wa Bongo Fleva ‘Navy Kenzo’ wanajiandaa kurudi na ujio wa album yao mpya. Hitmakers hao wa ngoma ya Why Now wamekuwa wakifanya vizuri kupitia digital platforms mbalimbali, na sasa tuitarajie “Dread and love album” ambayo tayari imekamilika kwa asilimia 70. Kwa mujibu wa Nahreel Kupitia insta story, amedokeza ujio wa album hiyo kwa kuandika ujumbe unaosomeka. “Dread & Love ALBUM 70% Loading” Hii inaenda kuwa album  ya NNE kwa Navy Kenzo, baada ya Hold me back iliyotoka mwaka wa 2015, Above inna Minute mwaka ya 2017 na Story of the African Mob iliyotoka mwaka 2020.

Read More