Nay wa Mitego, Billnass na Nandy Wazozana Hadharani

Nay wa Mitego, Billnass na Nandy Wazozana Hadharani

Mzozo mkali wa maneno umeibuka tena kwenye mitandao ya kijamii kati ya wasanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego, Billnass na mkewe Nandy, ukihusisha tuhuma za fitna, chuki na wivu wa maendeleo. Chanzo cha mvutano huo ni kauli ya Billnass aliyodai kuwa alipitia fitna za kutaka kufungwa kwa kesi ya wizi ambayo Nay wa Mitego alihusishwa nayo kwa kauli zisizo rasmi. Billnass, kupitia mahojiano yake na East Africa Radio, alionesha wazi kutoridhishwa na kile alichokiita hila zilizopangwa dhidi yake na watu aliowahi kuwachukulia marafiki. Baada ya maneno hayo, Nay wa Mitego hakusita kujibu kupitia sehemu ya maoni kwenye posti hiyo. Nay alimtaja Billnass kuwa ni msanii mjinga anayependa kiki bila mipaka na kumuita mwizi ambaye alistahili hata kifungo kwa tabia zake. “Acha nikupe unachotaka, wewe ni mwizi, ungeenda jela kwa tabia yako ya wizi. Nina kazi nyingi za kufanya, siwezi kushughulika na kukukandamiza wewe. Mgande Nandy ivyo ivyo ili usije ukaendelea na udokozi,” aliandika Nay wa Mitego. Kauli hiyo iliwasha moto zaidi pale mke wa Billnass, msanii Nandy, alipoamua kumjibu Nay moja kwa moja kwa hasira kali. Kupitia sehemu ya maoni, Nandy alimshutumu Nay kwa wivu na kumuita mvuta bangi, huku akidai kuwa ana chuki kutokana na kushindwa kimaisha. “Nay wa Mitego wewe cho…k…o, jina langu limeingiaje hapo? Mvuta bangi wewe! Una wivu wa maendeleo. Umejaribu kupambana umeshindwa, umebaki kuwa shabiki. Wa kuibiwa muibiwe nyie, na mnacho cha kuibiwa kwanza? Endelea na chaka zako ujikomboe, maisha upande huu mzito boob utasanda! Kithetheeee wewe, fyuu,” aliandika Nandy kwa hasira. Mashabiki kwenye mitandao wamegawanyika, baadhi wakimtetea Nay kwa kusema anasema ukweli bila uoga, huku wengine wakimtaka apunguze maneno ya matusi na wivu. Wengine wamewaomba wasanii hao warekebishe tofauti zao kwa hekima na busara badala ya kurushiana maneno hadharani. Kwa sasa, hakuna dalili za pande hizi kupoa, na mashabiki wanaendelea kufuatilia kwa karibu kuona ni nani atarushia dongo linalofuata.

Read More
 Nay wa Mitego adai wasanii wengi Tanzania wanatumia dawa za kulevya

Nay wa Mitego adai wasanii wengi Tanzania wanatumia dawa za kulevya

Mwanamuziki wa Hip Hop kutoka Tanzania, Nay wa Mitego amedai kuna wasanii wengi kwa sasa wanatumia dawa za kulevya ila bado hawajajulikana. Kupitia Insta Story amesema kama kuna la kufanya kupambana na hali hiyo ni sasa kabla mambo hayajawa mabaya zaidi. “Kwenye music industry kuna tatizo kubwa la wasanii kujiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya, now days imekuwa too much, yaani ni fashion, yaani wanaona ndio unyamwezi” amesema. “Ni vile tu bado hawajafikia hatua mbaya na kugundulika kufuatana na madhara ya dawa. Tahadhari kubwa kabla ya hatari, kama kuna cha kufanya ni sasa kabla ya janga” amesema Nay wa Mitego.

Read More
 NAY WA MITEGO AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA

NAY WA MITEGO AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA

Msanii wa Hiphop kutoka Tanzania Nay wa Mitego ameachia rasmi album yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake. Hitmaker huyo  wa ngoma ya “Atakuoa Nani” amewabarki mashabiki zake na  “Rais Wa Kitaa Album” ambayo ina jumla ya nyimbo 14 za moto, ikiwa na kutoka kwa wakali kama Alikiba, Marioo, Jux, Mejjah, Maua Sama, AY, Shammy, Runtown na Kelechi Africana. Album hiyo ambayo ni ya kwanza kwa mtu mzima Nay wa Mitego tangu aanze safari yake ya muziki kwa sasa inapatikana kwenye majukwaa yote ya ku-stream muziki mtandaoni. Utakumbuka mapema wiki hii iliyopita Nay wa Mitego alitajwa kuwania tuzo ya AFRIMA 2022 huko Nigeria kupitia vipengele viwili,  Best Artist Of The Year na Song Of The Year.

Read More
 NAY WA MITEGO ATANGAZA KUJITOA KWENYE TUZO ZA TANZANIA MUSIC AWARDS 2022

NAY WA MITEGO ATANGAZA KUJITOA KWENYE TUZO ZA TANZANIA MUSIC AWARDS 2022

Rapper kutoka nchini Tanzania Nay wa Mitego chini ya Uongozi wake wa Free Nation ametangaza rasmi kujitoa katika tuzo za muziki za Tanzania Music Awards. Kupitia taarifa ya wazi aliyowekwa mtandaoni, ameeleza sababu za kufikia maamuzi hayo ikiwa ni pamoja na kutokua na imani na kamati ya uchambuzi wa kazi yaani (academy) ambapo amewataka mashabiki zake kusitisha mchakato wa kumpigia kura kwenye kipengele cha msanii bora wa rap aliyochokuwa akiwania na na Professor Jay ,Rapcha, & Young Lunya . Aidha, tuzo hizo za muziki nchini Tanzania zinazoandaliwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) zinatarajiwa kutolewa Aprili mosi, mwaka wa 2022, huku vigezo vikubwa vilivyotumika kuwapata wasanii vikiwa ni wale waliopeleka kazi zao.

Read More
 SAKATA LA STEVE NYERERE NA SHIRIKISHO LA WANAMUZIKI TANZANIA LACHUKUA SURA

SAKATA LA STEVE NYERERE NA SHIRIKISHO LA WANAMUZIKI TANZANIA LACHUKUA SURA

Msanii wa Bongofeva Nay wa Mitego ameunga mkono kauli ya Mwana FA kutoa saa 48 kwa Shirikisho la Muziki Tanzania kuanza upya mchakato wa kumtafuta msemaji mpya kwa mujibu wa vigezo vilivyopo. Machi 21 wasanii mbalimbali wa muziki walikutana katika kikao jijini Dar es Salaam kujadili sakata hilo, huku wengi wakisema Steven Nyerere hawezi kuwa msemaji wala mhamasishaji wa muziki. “Kauli ya Mwana FA watu wasiichukulie kama kauli ya kibabe, kitemi na kutumia nafasi yake kama Mbunge lakini haya ni mawazo ya wasanii wengi ambao hawana nafasi ya kuongea na woga wakiamini Steve ni mtu wa ndani na ana-connection. wengi hatuungi mkono maamuzi ya shirikisho, na hiyo ni kauli yetu sio ya Mwana FA” “Kama mtu hana sifa za uongozi tukikubali atuongoze ni kama tumekubali bora yaende. yasiwe masaa 48, yawe hata masaa 24. Steve tunakupenda kama msanii wa kuchekesha lakini sio msemaji na afisa mipango wetu” amesema Nay. Hata hivyo, hapo awali Steve Nyerere alisema hana mpango wa kujiuzulu kama msemaji wa Shirikisho la wanamuziki Tanzania muda mchache tu baada ya wasanii hao kumpa saa 48 kufanya hivyo. “Nimeshateuliwa na kuchukua majukumu yangu kama Msemaji na Mratibu wa mipango ya shughuli za muziki na katu siwezi kung’atuka hata kwa dawa. Nawaambia tu, sijiuzulu na wala sitoki, Nina nia ya kuendeleza sanaa ya nchi hii,” amesema Steve Nyerere.

Read More
 RAPPER NAY WA MITEGO AWATOLEA UVIVU WATUMISHI WA MUNGU MASANJA MKANDAMIZAJI,MC PILI PILI NA NABII SHILLA

RAPPER NAY WA MITEGO AWATOLEA UVIVU WATUMISHI WA MUNGU MASANJA MKANDAMIZAJI,MC PILI PILI NA NABII SHILLA

Rapa mwenye utata nchini Tanzania Nay wa Mitego amewashutumu watumishi wa Mungu Masanja Mkandamizaji, Mc Pilipili na Nabii Shilla kuwa ni manabii wa uongo ambao kwenye vitabu vya dini wameandikwa. Kupitia Instastory yake kweny mtandao wa Instagram Nay wa Mitego ameandika  ujumbe unaosomeka “Mimi ndio maana sitakagu aya mambo ya Dini sijui nini.Yani Din imekuwa biashara hulia, eti Masanja Nae Mchungaji kuna mwingine yule tapeli Shilla sijui pumbavu kabisa. Huu ndio ule mwisho wa dunia ulioandikwa kwenye vitabu. Manabii wa uongo wamekuwa wengi mno”. Masanja na Mc Pilipili ni kati ya wachungaji waliotokea kwenye tasnia ya uchekeshaji na baadae kutangaza kumtumia Mungu kwa kufungua makanisa yao

Read More