NBA YoungBoy Kuachia Albamu Mpya Siku ya Uhuru Marekani
Rapa maarufu wa Marekani, NBA YoungBoy, ametangaza kupitia Insta Story yake kuwa ataachia albamu mpya tarehe 4 Julai 2025, siku ya Uhuru wa Marekani. Tarehe hiyo ina uzito mkubwa kihistoria, na tangazo hilo limeibua hisia tofauti kwa mashabiki wake. Wengi wamelitafsiri tangazo hilo kama njia ya kuadhimisha uhuru wake binafsi, baada ya kuachiwa kutoka gerezani Machi 2025, alikokuwa akitumikia kifungo cha mwaka mmoja kwa kosa la kumiliki silaha bila kibali. Ingawa hajafichua jina la albamu, mashabiki wanatarajia kazi hiyo itagusia maisha, mapambano, na matumaini yanayoendana na safari yake ya maisha. Kwa sasa, mashabiki wake wanasubiri kwa hamu ujio wa albamu hiyo, wakiamini itathibitisha uwezo wake wa kurudi kwa nguvu kwenye muziki baada ya changamoto nyingi.
Read More