PRODYUZA WA NDOVU KUU AWASHAURI VIJANA KUWEKA AKIBA

PRODYUZA WA NDOVU KUU AWASHAURI VIJANA KUWEKA AKIBA

Msanii wa muziki nchini Krispar amewataka vijana kujenga tabia ya kuweka akiba kwa kuwa itawasaidia wakati wa matatizo. Katika mahojiano yake na Kiss TV Krispar kuu amesema vijana wengi wamekuwa na mazoea ya kutumia pesa kwenye masuala ya starehe na anasa, jambo ambalo limepelekea baadhi yao kutotimiza malengo yao katika maisha. Msaniii huyo amesema licha ya kwamba kuweka akiba ni ngumu kwa baadhi ya vijana ila wanapaswa kuwa na nidhamu kwenye matumizi ya pesa kuondoa gharama isioyokuwa na msingi. Sanjari na hilo Hitmaker huyo wa ngoma ya “Ndovu Kuu” amewashauri wasanii kuwa na timu itakayowasaidia kusukuma muziki wao badala ya kuingia mikataba isiyoeleweka na lebo za muziki ambazo zinawafunga kisanaa. Utakumbuka Krispar alipataa umaarufu nchini kipindi cha corona alipoachia wimbo wake uitwao ndovu kuu licha ya kuwa kwenye tasnia muziki kwa kipindi cha miaka 7.

Read More
 NDOVU KUU AWATOLEA UVIVU WATOTO WA KIKE

NDOVU KUU AWATOLEA UVIVU WATOTO WA KIKE

Rapa Ndovu Kuu ametoa ya moyoni kuhusu watu wanafiki ambao mara nyingi huwafuata marafiki zao kwa ajili ya vitu wanavyomiliki katika maisha. Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram rapa huyo amewataka akina watu sampuli hiyo kuwaamini marafiki zao kwa uhalisia wao wa maisha na sio kwa vitu vya thamani wanavyovimiliki kwa wakati huo. Mkali huyo wa ngoma ya “Maggie wa nyumbani” amesema maisha ubadilika haraka, hivyo mali ambayo watu wanamiliki kwa sasa huwa inaisha pia. Hata hivyo hajabainika ni kitu gani kilimpelekea rapa huyo kutoa kauli hiyo ila wajuzi wa mambo kwenye mitandao ya kijamii wanahisi huenda mahusiano ya kimapenzi ya ndovu kuu yameingiwa na ukungu.

Read More
 BIEN WA SAUTI SOL ATOA OFA  KWA YEYOTE ATAKAYEMREJESHEA SIMU YAKE ILIYOIBIWA

BIEN WA SAUTI SOL ATOA OFA KWA YEYOTE ATAKAYEMREJESHEA SIMU YAKE ILIYOIBIWA

Member wa Sauti Sol, Bien ameahidi kutoa ofa ya shillingi elfu 50 kama zawadi kwa yeyote atakayemrudishia simu yake ambayo juzi kati iliibiwa katika ukumbi wa burudani wa Carnivore kwenye onesho la NRG Wave Concert. Kupitia ukurasa wake wa Twitter Bien ameandika ujumbe wa masikitiko kwa kusema kwamba aliibiwa simu aina ya Infinix Note 11 Pro na vifunguo vya gari aina ya Porsche Cayenne ambapo amedai kuwa simu yake ilikuwa na data muhimu ya album mpya ya Sauti Sol ambayo inatarajiwa kuingia sokkoni mwezi Aprili mwaka huu. Hitmaker huyo wa “Mbwe Mbwe” ameenda mbali zaidi na  kutania kuwa hangekaa vibaya watu wangemuibia hata mke wake Chiki Kuruka huku akisisitiza kutoa zawadi ya shillingi elfu 50 kwa yeyote atakayemrudhishia simu pamoja na vifunguo vya gari. Sanjari na hilo msanii Ndovu Kuu amethibitisha kuibiwa simu kwenye onesho la NRG Wave Concert lilofanyika katika ukumbi wa Carnivore ambapo pia ameahidi kutoa zawadi kwa yeyote atakayemregeshea simu yake.

Read More