MASHABIKI WAMJIA JUU MKE WA NE-YO KWA KUDANGANYA AMEACHANA NA MUME WAKE

MASHABIKI WAMJIA JUU MKE WA NE-YO KWA KUDANGANYA AMEACHANA NA MUME WAKE

Baada ya kashfa nzito inayomkabili Ne-yo, iliyovujishwaa na mkewe bibie Crystal Smith mwishoni mwa wikiendi kuhusu mwanamuziki huyo kujihusisha na vitendo vya usaliti, kwa kutoka kimapenzi na wanawake wenye kufanya biashara ya kuuza miili yao , na kisha Crystal kuweka wazi maamuzi yake kuwa sio mke tena wa Ne-yo, mapya yaibuka! Kwenye moja ya video siku jana ambayo Crystal aliiposti kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa ndani ya gari yake anasikiliza muziki, mashabiki wakagundua kwenye kidole chake kuna pete ya ndoa jambo ambalo mashabiki wamelitafsiri kuwa madai ya kuachana sio ya kweli kwani alikuwa anatafuta kuzungumziwa. Aidha, komenti za kumponda zilikuwa ni nyingi zikimshutumu kwamba anatafuta kuongelewa, nae Crystal hakubaki nyuma aliweza kuzijibu chache akisema kwamba kuachana na Ne-yo hakumzuii yeye kuvaa pete hiyo ambayo ameitaja kuwa ni ya gharama kubwa iliyonakshiwa na madini ya Almasi. Utakumbuka Ne-yo na Crystal Smith, katika ndoa yao wamefanikiwa kupata watoto watatu, ambao ni Shaffer (6), Roman (3) na Isabella mwenye umri wa miezi 13.

Read More
 NEYO AFUNGUKA KUHUSU NDOA YAKE KUVUNJIKA

NEYO AFUNGUKA KUHUSU NDOA YAKE KUVUNJIKA

Mwanamuziki kutoka Marekani Ne-Yo ametoka hadharani na kuzungumzia Jambo ambalo jana mkewe Crystal Smith alilileta mtandaoni akisema ndoa yake na Mwanamuziki huyo imevunjika kutokana na vitendo vya usaliti. Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Ne-Yo ameomba faragha katika kulishughulikia jambo hili kwa maslahi ya watoto wake na familia yake kwa ujumla. “Kwaajili ya watoto wetu na familia yangu kwa ujumla nitazitatua changamoto tunazozipitia kwa usiri. Mambo ya familia hayapaswi kuwekwa hadharani. Nawaomba muheshimu faragha ya familia yangu kwa sasa” Crystal Smith juzi alishusha madai kwamba Ne-Yo amekuwa akifanya vitendo vya usaliti kwa kutoka na wanawake wanaojiuza tena bila kutumia kinga.  

Read More