NELLY AOMBA RADHI KUFUATIA KUVUJA KWA VIDEO IKIMUONESHA AKIFANYA NGONO YA MDOMO

NELLY AOMBA RADHI KUFUATIA KUVUJA KWA VIDEO IKIMUONESHA AKIFANYA NGONO YA MDOMO

Mwanamuziki nyota kutoka nchini Marekani Nelly ameomba radhi hadharani kufuatia kuvuja kwa video ambayo inamuonesha akiwa anafanya ngono ya mdomo (Oral Sex) na mwanamke mmoja. Video hiyo ilipostiwa kwenye akaunti ya instagram ya Nelly Februari 8 mwaka huu na ilifutwa haraka lakini tayari ilikuwa imeshanaswa na kusambazwa mtandaoni. Kupitia Instagram page yake Nelly ameandika kwa masikitiko “Ninaomba radhi kwa msichana huyu na familia yake, hiki ni kitendo ambacho hakikubaliki kwake hata kwenu pia. Hii ilikuwa ni video ya zamani ambayo ilikuwa ya faragha na haikukusudiwa kwenda kwenye hadhira.”

Read More
 MASHABIKI WAMSHAMBULIA NELLY KISA KUMPA ZAWADI NDOGO MWANAMKE ALIYEMRUDISHIA MAMILIONI

MASHABIKI WAMSHAMBULIA NELLY KISA KUMPA ZAWADI NDOGO MWANAMKE ALIYEMRUDISHIA MAMILIONI

Mashabiki wamemtolea na kumtupia maneno mwanamuziki Nelly kutoka nchini Marekani baada ya stori ya mwanamke mmoja ambaye alipewa shilling 11,388 za kenya kama zawadi baada ya kuokota na kulirudisha begi la Nelly lililokuwa na zaidi ya shilling milllioni 11 za kenya. Hata hivyo Nelly aliibuka na kukanusha taarifa hiyo kupitia ukurasa wa instagram ambao uliweka video hiyo. Kwenye uwanja wa comment aliandika hajapoteza begi na wala hafahamu chochote kuhusu begi hilo linaloongelewa kwenye mitandao ya kijamii.

Read More
 LEO KATIKA HISTORIA NOVEMBA 2, ALIZALIWA STAA WA MUZIKI WA RNB KUTOKA MAREKANI, NELLY.

LEO KATIKA HISTORIA NOVEMBA 2, ALIZALIWA STAA WA MUZIKI WA RNB KUTOKA MAREKANI, NELLY.

Siku kama ya leo Novemba 2 mwaka wa 1974 alizaliwa Staa wa muziki wa RnB na Hiphop kutoka Marekani, Nelly. Jina lake halisi ni Cornell Iral Hayness JR. na alizaliwa huko Austin, Texas nchini Marekani ambako alianza muziki mwaka wa 1993 akiwa na kundi la Lunatics lakini mwaka wa 1999 alisaini mkataba na lebo ya muziki ya Universal Records. Akiwa chini ya lebo ya universal mwaka wa 2000, Nelly aliachia album yake ya kwanza kama msaani wa kujitegemea iitwayo Country Grammar,album hiyo ilifanikiwa kushika namba 3 kwenye chati ya BillBoard 200 lakini pia iliweza kushika namba moja kwenye chati hiyo. Baada ya album ya Country Grammar kuuza zaidi nakala millioni 8.4 nchini Marekani, Nelly aliachia album yake ya pili iitwayo Nellyville mwaka wa 2002, album ambayo ilikuwa na mikwaju kama  Dillemma,Work it na Air Forces Ones. Mwaka wa 2004 Nelly aliachia album mbili kwa mpigo,ambazo ni Sweat  na Suit album ambazo zilifanya vizuri kwenye chati mbali mbali za muziki nchini Marekani. Album ya Sweat ilifanikiwa kushika namba mbilii kwenye chati ya Billboard 200 na kuuza ya nakala 342,000 ndani ya wiki moja tangu iachiwa kwake huku album  ya Suit  ikishika namba moja kwenye Billboard 200 na kuuza nakala 396,000 ndani ya wiki moja. Mwaka wa 2008 Nelly aliachia album yake ya tano iiitwayo Brass Knuckles ikafuatwa na album yake ya sita  iitwayo 5.0 album ambayo ilikuwa ngoma kama Just A Dream, ngoma ambayo ilifanikiwa kufikia viwango vya mauzo ya Platimuz mara tatu nchini Marekani. Hata hivyo tangu aanze muziki mwaka wa 1993 Nelly ameshafanya jumla ya album  saba ya muziki,EP tatu, Mixtape mbili,Singles 48 na album mbili za nyimbo ambazo zilizotoka na ambazo pia hazikutoka. Kutokana na mafanikio yaliyopata kwenye muziki wake, Nelly ameteuliwa kushiriki kwenye tuzo mbali mbali nchini marekani na ameshinda tuzo mbili za Grammy. Kando na muziki, Nelly ameigiza kwenye filamu nchini marekani ikiwemo Snipes ya mwaka wa 2001,The Longest ya mwaka wa 2005 na Reach Me ya mwaka wa 2014.

Read More