RASMI: NICCAH THE QUEEN ATHIBITISHA KUACHANA NA DJ SLAHVER
Msanii wa nyimbo za injili nchini Niccah The Queen ameweka wazi kuwa yeye na mchumba wake DJ Slahver wameachana. Niccah amebainisha hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amesema amechukua maamuzi ya kuachana na mpenzi wake huyo baada ya kuafikia makubaliano ya pamoja huku akimtakia kila la kheri kwenye maisha yake mpya. Hata hivyo Niccah The Queen hajatoa maelezo zaidi kuhusu kiini cha uhusiano wake na DJ Slahver kuvunjika ila walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wamehoji kuwa huenda msanii huyo anatengeza mazingira ya kumzungumziwa nchini Kenya kabla ya ujio wa ngoma yake mpya Ikumbukwe kuwa penzi la Niccah The Queen na DJ Slahver lilianza rasmi mwishoni mwa mwaka jana miezi kadhaa baada ya kuachana na aliyekua mpenzi wake Dkt. Ofweneke.
Read More