Nicholas Kioko na Wambo Watumia Helikopta Kwenye Gender Reveal, Watangaza Wanatarajia Mtoto wa Kike

Nicholas Kioko na Wambo Watumia Helikopta Kwenye Gender Reveal, Watangaza Wanatarajia Mtoto wa Kike

Wanandoa maarufu mitandaoni nchini Kenya, Nicholas Kioko na Wambo Ashley, wamevutia hisia za wengi baada ya kuandaa sherehe ya kifahari ya kutangaza jinsia ya mtoto wao, wakitumia helikopta (chopper) katika tukio lililojaa burudani. Kupitia video na picha walizoshiriki mitandaoni, wanandoa hao walionekana wakiwa katika hafla hiyo ya kipekee ambapo helikopta iliruka juu ya eneo la tukio na kumwaga moshi wa rangi ya pink, ishara iliyothibitisha kuwa wanatarajia mtoto wa kike. Nicholas Kioko na Wambo Ashley wameelezea furaha yao kubwa kwa baraka hiyo, wakishukuru Mungu na kuwashukuru mashabiki wao kwa upendo na sapoti waliyoendelea kuwaonesha tangu walipotangaza ujauzito huo. Gender reveal hiyo ya kifahari imezua mjadala mitandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakiwapongeza kwa ubunifu na uwezo wao wa kuandaa tukio la kiwango cha juu, huku wengine wakijadili mwenendo unaokua wa watu mashuhuri kutumia gharama kubwa katika sherehe za binafsi.

Read More
 Nicholas Kioko Apinga Madai ya Kuachana na Wambo Ashley

Nicholas Kioko Apinga Madai ya Kuachana na Wambo Ashley

Mtangazaji na content creator Nicholas Kioko amejitokeza wazi kukana tetesi za kuvunjika kwa mahusiano yake na mpenzi wake Wambo Ashley. Kupitia InstaStories, Kioko alifafanua kuwa mapenzi yao bado ni imara na hayatikisiki, akiongeza kwa utani kuwa hakuna uchawi au presha ya mitandaoni itakayomfanya amuache Wambo. Alisisitiza kuwa wao ni moja ya wapenzi wanaoendana zaidi na kwamba wanaotumai kuona wakiachana “watangoja sana.” Uvumi huu ulianza baada ya shabiki mmoja kudai kuwa Kioko na Wambo wangekuwa wanandoa wa pili kuachana, kufuatia misukosuko ya mahusiano iliyoikumba wanandoa wa karibu nao akiwemo Commentator 254 na Moureen pamoja na Vinny Flava na Ng’ang’a. Hata hivyo, Kioko ameweka wazi kuwa yeye na Wambo hawaguswi na tetesi hizo na mapenzi yao yanaendelea kuimarika.

Read More