Bahati athibitisha kufanya kolabo na Nick Minaj

Bahati athibitisha kufanya kolabo na Nick Minaj

Mwanamuziki wa Kenya Bahati amethibitisha kufanya kazi ya pamoja na Rapa kutoka Marekani Nicki Minaj. Bahati ameweka taarifa hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram akifichua kuwa wataachia rasmi wimbo wao mwaka 2023. “2023, Bahati na Nicki Minaj imethibitishwa..,” ameandika kupitia Insta stori yake. Baadhi ya Mashabiki wametilia shaka habari hizo ikizingitiwa kuwa mwanamuziki huyo amekuwa akijihusisha sana na kiki kwa ajili ya kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa kwenye vyombo vya habari. Kwa upande mwingine baadhi wamesema kuwa taarifa ya Bahati kufanya kolabo na Nicki Minaj inaweza kuwa na ukweli kwa sababu amekuwa akifanya kazi kwa bidii kwenye muziki wake. Hata hivyo mashabiki wake sasa wanasubiri kwa hamu 2023 wakiwa na matumaini makubwa kuwa wimbo huo utakuwa mkali zaidi . Nicki Minaj ambaye ni mmoja wa marapa bora zaidi wa kike duniani, kolabo hii na Bahati ikitoka inakuwa ni kolabo yake ya pili kushirikishwa na mwanamuziki toka Afrika baada ya Davido (Nigeria) kwenye wimbo “Holy Ground” uliotoka mwaka 2020.

Read More
 MUME WA NICK MINAJ AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 3 JELA

MUME WA NICK MINAJ AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 3 JELA

Mume wa Nicki Minaj, Kenneth Petty amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu chini ya Uangalizi wa Mahakama pamoja na Kifungo cha nyumbani mwaka mmoja baada ya kukiri kushindwa kujisajili kama mkosaji wa Kingono (Sex Offender) katika Jimbo la California mwaka 2020. Kwa mujibu wa Mwanasheria wa Serikali, Mahakama pia imemtaka alipe faini ya dollar ($55,000). Petty mwenye umri wa miaka 44, alihitajika kujisajili kama mkosaji wa Kingono baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka msichana wa miaka 16 mwaka 1995 ambapo alikaa Jela miaka 4.    

Read More