Nicki Minaj Apata Msaada wa Kisiasa Kufuatia Vitisho vya MackWop

Nicki Minaj Apata Msaada wa Kisiasa Kufuatia Vitisho vya MackWop

Mbunge wa Marekani Anna Paulina Luna amethibitisha kuwa amewasiliana moja kwa moja na msanii wa rapa Nicki Minaj baada ya kauli za kutishia usalama wake kutolewa na MackWop, mshirika wa lebo ya TDE. Hatua hiyo imechukuliwa kama sehemu ya kuhakikisha usalama wa Minaj kufuatia matamshi ambayo yalionekana kama tishio la moja kwa moja dhidi ya maisha yake. Kauli ya MackWop, iliyotolewa kupitia livestream, ilieleza kuwa Minaj asipojichunga anaweza kuishia kama rafiki yake anayedhaniwa kuwa ni Tory Lanez, ambaye aliripotiwa kudungwa visu akiwa gerezani. Kauli hiyo imeibua hofu na taharuki miongoni mwa mashabiki na wanasiasa, na kuchochea mjadala kuhusu usalama wa wasanii katika tasnia ya burudani. Chanzo cha mvutano huu kilianza baada ya Minaj kuonyesha dhamira ya kufichua maovu aliyotendewa na MackWop wakati walipokuwa wakifanya kazi pamoja. Hatua hiyo haikupokelewa vyema na meneja huyo wa zamani, hali iliyochochea kauli za vitisho na mashambulizi ya maneno mtandaoni. Katika mkondo huo huo wa sintofahamu, msanii SZA pia alijikuta akihusishwa na ugomvi huo baada ya kuonekana kama anamrushia vijembe Minaj kupitia mafumbo kwenye mitandao ya kijamii. Minaj hakusita kumjibu kwa matusi na maneno makali, hali iliyoongeza moto katika mvutano huo wa hadharani. Mbunge Luna, akielezea msimamo wake, amesema kuwa vitisho vya aina hii haviwezi kufumbiwa macho, na ametoa hakikisho kuwa hatua zitachukuliwa ili kulinda wasanii dhidi ya ukatili wa kimfumo ndani ya tasnia ya muziki. Wito umetolewa kwa wadau wa muziki kuhakikisha mazingira salama, huru na ya haki kwa kila msanii bila woga wa kulipiziwa kisasi.

Read More
 Nicki Minaj Atishia Kufichua Ukweli kwa FBI na CIA Kufuatia Kisa cha Tory Lanez Kudungwa Kisu

Nicki Minaj Atishia Kufichua Ukweli kwa FBI na CIA Kufuatia Kisa cha Tory Lanez Kudungwa Kisu

Malkia wa muziki wa Hiphop duniani Nicki Minaj ameibua taharuki baada ya kudai kuwa anahisi tukio la Tory Lanez kudungwa kisu gerezani lilikuwa njama ya makusudi. Nicki sasa anasema yuko tayari kuzungumza na mashirika ya upelelezi ya Marekani, FBI na CIA, kuhusu kile anachodai kuwa ni mtandao wa vitisho vinavyohusisha watu wenye ushawishi mkubwa kwenye tasnia ya burudani. Nicki Minaj ameeleza kuwa maneno yaliyotolewa na MackWop, mshirika wa kundi la muziki la TDE, yanaonyesha wazi viashiria vya vitisho dhidi yake na vina uhusiano wa moja kwa moja na shambulio dhidi ya Tory. Aidha, amelaumu kile anachokiita ni tabia ya baadhi ya watu ndani ya tasnia ya muziki ambao wanajiona wako juu ya sheria na sasa wameanza kutoa vitisho hadharani. Tory Lanez, anayehudumia kifungo cha miaka 10 kwa kosa la kumpiga risasi msanii mwenza Megan Thee Stallion, alishambuliwa na kudungwa kisu mara 14 akiwa katika Gereza la Tehachapi, California, mwezi Mei 2025. Alipata majeraha mabaya ikiwemo mapafu kudidimia, pamoja na majeraha usoni, mgongoni na kichwani. Tukio hilo limezua maswali mengi kuhusu usalama wa wafungwa mashuhuri.

Read More
 Nicki Minaj Amtukana SZA Hadharani Bila Huruma, Mashabiki Wabaki Midomo Wazi

Nicki Minaj Amtukana SZA Hadharani Bila Huruma, Mashabiki Wabaki Midomo Wazi

Mapambano ya maneno kati ya mastaa wawili wakubwa wa muziki, Nicki Minaj na SZA, yamezua taharuki mitandaoni baada ya wawili hao kubadilishana kauli kali kupitia mtandao wa X (zamani Twitter). Kulingana na taarifa kutoka Page Six, mzozo huo ulianza baada ya Nicki kumshutumu meneja wa zamani wa SZA, Terrence “Punch” Henderson, kwa kile alichokiita udhalilishaji dhidi yake. Nicki Minaj aliandika mfululizo wa jumbe akidai kuwa ana ushahidi (“receipts”) wa vitendo vya dhuluma kutoka kwa Punch, na kutumia hashtag ya kushangaza: #JusticeForDemoree. Ingawa hakumtaja moja kwa moja SZA katika ujumbe huo wa awali, SZA alionekana kujibu kwa ujumbe wa mafumbo akisema, “Mercury retrograde… don’t take the bait lol silly goose.”, ambao mashabiki wengi waliutafsiri kama vijembe dhidi ya Nicki. Hilo halikumfurahisha Nicki, ambaye alilipuka na kumtaja SZA kama “kitoto,” na kudai kuwa nyimbo zake zingetoweka leo na hakuna mtu angekosa. Aliongeza matusi ya moja kwa moja akisema SZA “anasikika kama mbwa aliyekufa.” SZA hakubaki kimya. Alijibu kwa kusema, “I don’t give a f** bout none of that weird s*** you popping… I’m good in real life.”* Alisisitiza kuwa licha ya mashambulizi ya mitandaoni, anaendelea kupata mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki kwenye ziara zake za kimataifa. Mashabiki wamegawanyika mitandaoni, wengine wakimtetea SZA kwa kuwa mtulivu na wengine wakimuunga mkono Nicki kwa kusimama kidete dhidi ya wale anaodai walimdhulumu. Kufuatia mvutano huu, inaonekana kuwa mgogoro kati ya Nicki Minaj na SZA unaweza kuwa na athari pana zaidi kwenye tasnia ya muziki, hasa ikizingatiwa kuwa wawili hao walikuwa wakihusishwa na uwezekano wa kushirikiana hapo awali. Kwa sasa, mashabiki wanasubiri kuona iwapo mzozo huu utazidi kupamba moto au kama pande zote zitachukua hatua ya kusuluhisha tofauti zao.

Read More
 Nicki Minaj Afunguka Kuhusu Sakata la Deni la Tidal

Nicki Minaj Afunguka Kuhusu Sakata la Deni la Tidal

Mwanamuziki maarufu wa hip hop, Nicki Minaj, ameibua shinikizo kwa rapa na mwekezaji, Jay-Z, akidai kuwa anamdai kati ya dola milioni 100 hadi 200 baada ya kuuza mtandao wa kusikiliza muziki wa TIDAL mwaka 2021. Katika madai haya ambayo yamezua gumzo mitandaoni, Nicki amesema kuwa alikuwa mmoja wa wasanii wa awali kumiliki sehemu ya mtandao huo na alifanya juhudi kubwa zaidi za kuitangaza TIDAL, ikiwemo kuliko msanii mwenzake, Beyoncé, wakati wa uzinduzi wa mtandao huo. “Nilipambana sana kutangaza TIDAL, zaidi hata ya Beyoncé,” alisema Nicki. Nicki anadai kuwa wakati Jay-Z aliuza mtandao wa TIDAL kwa kampuni ya Square, inayomilikiwa na Jack Dorsey aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Twitter, kwa kiasi cha dola milioni 300, wasanii wenzake walilipwa kati ya dola milioni 8 hadi 9 kila mmoja, lakini yeye hakuambulia hata senti. Zaidi ya hayo, Nicki amesema alipokea ofa ya dola milioni 1 (takriban Shilingi bilioni 2.6) ili kutuliza madai haya, lakini alikataa. “Nilipewa ofa ya dola milioni moja ili ninyamaze, lakini sikuikubali. Mashabiki wangu wanastahili kujua ukweli,” alisema Nicki. Madai haya yamepokelewa kwa msisimko mkubwa, huku mashabiki wake, maarufu kama Barbz, wakimpongeza kwa kuonyesha maadili ya kuhimiza uwazi na haki, hasa kwa kuwa Nicki alichangia kwa kiasi kikubwa katika kuifanya TIDAL kuwa mtandao maarufu. Kwa historia, Jay-Z alinunua TIDAL mwaka 2015 kwa dola milioni 56 na baadaye kuuza hisa nyingi za mtandao huo kwa kampuni ya Square kwa dola milioni 297 (kama Shilingi bilioni 689+). Wasanii wengine wamiliki wa mtandao huo ni pamoja na Alicia Keys, Beyoncé, J. Cole, Kanye West, Lil Wayne, Rihanna, T.I, pamoja na Nicki Minaj mwenyewe. Madai haya yanazua mjadala mzito katika tasnia ya muziki na uwekezaji, huku wengi wakisubiri maelezo rasmi kutoka kwa Jay-Z na kampuni ya Square kuhusu madai ya Nicki Minaj.

Read More
 Nicki Minaj afichua kuwa alifikiria kuacha muziki kutokana na ukosoaji na changamoto za kazi

Nicki Minaj afichua kuwa alifikiria kuacha muziki kutokana na ukosoaji na changamoto za kazi

Rapa maarufu Nicki Minaj amefunguka kuhusu changamoto kubwa alizokumbana nazo katika maisha yake ya muziki. Katika mahojiano na Vogue Italia, Minaj amesema kuwa mara kadhaa alifikiria kuacha kabisa kazi kutokana na ukosoaji wa mara kwa mara na shinikizo la umaarufu. Amesema kuwa licha ya mawazo hayo ya kukata tamaa, aliamua kuendelea kusonga mbele. “Nimesikia ukosoaji mwingi kuhusu mimi na kazi yangu. Nimewaza kuacha muziki mara nyingi, lakini najivunia kusimama imara na kuendelea.”, Minaj alisema Katika maelezo yake, Minaj amegusia namna alivyolazimika kuchelewesha uamuzi wa kuwa mama ili kutimiza ndoto zake na kusaidia familia. Anasema japokuwa baadhi ya wanawake hawajuti kuchelewa kuanzisha familia, kwake ilikuwa ni hali ngumu iliyoambatana na majuto fulani. “Kama mwanamke, nilichelewesha kuwa mama, jambo ambalo baadhi ya wanawake katika tasnia yetu wamelikumbana nalo pia,” alisema. “Wengine hawajutii kuchelewa, lakini mimi niliona gharama zake.” Akiwa sasa mama wa mtoto mwenye umri wa miaka minne, kupitia ndoa yake na Kenneth Petty, Minaj anakiri kuwa alikosa nyakati nyingi muhimu katika maisha kama vile sikukuu, mapumziko na hatua muhimu za kibinafsi, kutokana na kujitolea kikamilifu katika kazi yake ya muziki. Licha ya hayo, anaeleza kuwa anajitahidi kumpa mwanawe maisha yenye utulivu na fursa alizokosa yeye mwenyewe alipokuwa anatafuta mafanikio. “Nililazimika kukosa sherehe za familia na likizo kwa sababu ya kazi yangu. Gharama kubwa ilikuwa kukosa maisha ya kawaida,” aliongeza. Kauli hii ya Minaj imepokelewa kwa hisia mseto mtandaoni, huku mashabiki wakimpongeza kwa ujasiri wake na uwazi katika kushiriki changamoto za maisha yake binafsi. Wengine wamelitumia tukio hili kuibua mjadala kuhusu gharama za umaarufu kwa wanawake katika tasnia ya burudani.

Read More
 Nicki Minaj Aonyesha Upendo kwa Wasanii Chipukizi

Nicki Minaj Aonyesha Upendo kwa Wasanii Chipukizi

Malkia wa muziki wa Rap kutoka Marekani Nicki Minaj ameonyesha upendo kwa kizazi kipya cha wasanii katika mahojiano mapya na Vogue Italia. Rapa huyo mwenye mafanikio makubwa alimtaja Sabrina Carpenter kama msanii anayemvutia kwa ubunifu na mvuto wa kipekee, akieleza kuwa aligundua kipaji chake hivi karibuni licha ya Carpenter kuwa kwenye muziki kwa muda. “Sabrina Carpenter… ni kama pumzi safi ya hewa,” alisema Minaj. “Sikujua kwamba alikuwa kwenye game kwa muda mrefu kiasi hicho nilipoanza kumsikiliza.” Aidha, alimsifu Billie Eilish kwa ubunifu wake wa kipekee katika muziki wa kisasa. Licha ya kutotajwa rasmi, Eilish anasikika katika utangulizi wa albamu ya Nicki Pink Friday 2, ishara kwamba uhusiano wa kisanii kati yao tayari umeanza kuchipua. “Napenda kila kitu anachofanya. Ni msanii wa kipekee sana.”, Nicki alisema. Nicki pia alimpongeza Skeng, msanii wa dancehall kutoka Jamaica, kama mmoja wa wanaoleta ladha tofauti kwenye muziki wa sasa. Akizungumzia mitandao ya kijamii, Nicki alieleza kuwa ingawa ina athari kubwa katika kujenga majina ya wasanii, bado kipaji halisi hujitokeza hata bila ushawishi wa mtandao. “Superstar ni superstar, iwe na mitandao ya kijamii au bila.”, Alilisitiza Minaj. Mashabiki sasa wana matumaini ya kuona mashirikiano ya wazi kati ya Nicki na wasanii hao aliowataja hasa Carpenter, ambaye bado hawajafanya kazi pamoja.

Read More
 NICK MINAJ AMSHTAKI YOUTUBER NOSEY HEAUX KWA KUMCHAFUA MTANDAONI

NICK MINAJ AMSHTAKI YOUTUBER NOSEY HEAUX KWA KUMCHAFUA MTANDAONI

Rapa kutoka Marekani Nicki Minaj amemfungulia mashtaka mtengeneza maudhui ya YouTube (Marley Green) maarufu kama Nosey Heaux mara baada ya kuibua madai kuwa rapa huyo anatumia dawa za kulevya. Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama, Nicki Minaj amedai Nosey alipakia video hiyo juzi Jumatatu na kumchafua kwa shutuma hizo ikiwemo pia kumtaja mtoto wake wa kiume kwamba atakuwa mbakaji kama baba yake, Kenny Petty. Minaj amedai fidia ya zaidi ya Shillingi Millioni 9 za Kenya lakini pia ametishia kulichukua Jina la ‘Nosey Heaux’ ambalo linatumika kibiashara, kama mwanadada huyo blogger akishindwa kulipa pesa hizo. Nicki Minaj pia ameweka wazi msimamo wake kwamba yeyote ambaye atasambaza habari za uwongo kumuhusu basi atawajibishwa.

Read More
 IGGY AZALEA AKANUSHA KUWA KWENYE UGOMVI NA NICKI MINAJ

IGGY AZALEA AKANUSHA KUWA KWENYE UGOMVI NA NICKI MINAJ

Rapa Iggy Azalea amekanusha kuwa kwenye bifu na Nicki Minaj, Iggy ameibuka na kujibu shutuma hizo kufuatia Tweet ya New York Post ambayo ilianika wasanii wa Kike ambao wamewahi kuwa kwenye ugomvi na Nicki Minaj akiwemo Cardi B, Mariah Carey na Miley Cyrus. Iggy alishuka kwenye comment na kukanusha hilo kwa kusema kwanini amewekwa kwenye orodha hiyo wakati anaamini pamoja hawajahi kusemeana vibaya. Fahamu kwamba wawili hao walianza kuhusishwa kuwa kwenye bifu mwaka 2014 baada ya hotuba ya Nicki Minaj wakati akipokea Tuzo ya BET kutafsiriwa kuwa alimtolea uvivu mkali huyo wa ngoma ya “Fancy”.

Read More
 AMBER ROSE AFUNGUKA SAKATA LA KANYE WEST NA NICKI MINAJ KUPITIA WIMBO WA MONSTER

AMBER ROSE AFUNGUKA SAKATA LA KANYE WEST NA NICKI MINAJ KUPITIA WIMBO WA MONSTER

Verse ya Nicki Minaj kwenye ngoma ya Kanye West “Monster” ya mwaka 2010 ilikuwa ya moto sana ingawa YE hajawahi kufurahishwa na mauaji ya mrembo huyo kwenye ngoma hiyo. Sasa Amber Rose ambaye ndiye alimleta Nicki Minaj studio kuifanya verse hiyo, amerudi tena na kufunguka mengi kuhusu sakata hilo. Kwenye mahojiano yake na Podcast ya (Higher Learning) Amber amesema Kanye West aliwahi kumtamkia wazi kuwa, kwanini umeniletea mtu ambaye amekuja kuniua kwenye ngoma yangu? YE: “How the f*ck did you bring in a b*tch that killed me on my own song?” Amesema. Utakumbuka mwanamitindo na mwigizaji kutoka Marekani Amber Rose aliwahi kukaririwa mwaka 2018 akisema YE alibaki kidogo aifute verse hiyo.

Read More
 NICKI MINAJ AMFIKIA RIHANNA KWA IDADI YA VIDEO ZILIZOFIKISHA VIEWS BILLIONI 1 YOUTUBE

NICKI MINAJ AMFIKIA RIHANNA KWA IDADI YA VIDEO ZILIZOFIKISHA VIEWS BILLIONI 1 YOUTUBE

Malkia wa muziki wa Hiphop kutoka Marekani Nicki Minaj amemfikia Rihanna kwa idadi ya video ambazo zimefikisha Jumla ya views Bilioni 1 kwenye mtandao wa YouTube. Minaj amefikisha video 8, sawa na Rihanna. Rapa huyo amefikia hatua hiyo kupitia video aliyoshirikishwa na Justin Bieber “Beauty And A Beat” ambayo pia inamfanya Justin Bieber kufikisha video 11 zenye idadi hiyo ya watazamaji.

Read More