NIKKI MBISHI AACHIA ALBUM YAKE MPYA- ‘WELCOME TO GAMBOSHI’

NIKKI MBISHI AACHIA ALBUM YAKE MPYA- ‘WELCOME TO GAMBOSHI’

Hatimaye Rapa kutoka nchini Tanzania Nikki Mbishi ameachia rasmi album yake mpya aliyokuwa ikisubiriwa na mashabiki zake. Hitmaker huyo  “Babu Talent” amewabarki mashabiki zake na  ‘Welcome to Gamboshi’ album ambayo ina jumla ya nyimbo 22 za moto, ikiwa na kolabo 12  kutoka kwa wakali kama Ally Choki, P Mawenge, Wakazi, Tk Ndendezi, Zaiid pamoja na wengine wengi. Album hiyo kwa sasa inapatikana kwenye majukwaa yote ya ku-stream muziki duniani na ina ngoma kama Welcome to Gambosh, Party ya Uwaki, Wazee Wabishi, Wanyonge,  Nenda na nyingine nyingine. Album ya “Welcome to Gamboshi” inazifuata album kama Sauti ya Jogoo, Ufunuo wa unju na Sam Magoli kutoka kwa mtu mzima Nikki Mbishi. .

Read More
 NIKKI MBISHI:  MARIOO ALISTAHILI KUPEWA MIRABAHA NA COSOTA KUTOKA KAZI ZAKE KUPIGWA SANA KWENYE MEDIA

NIKKI MBISHI: MARIOO ALISTAHILI KUPEWA MIRABAHA NA COSOTA KUTOKA KAZI ZAKE KUPIGWA SANA KWENYE MEDIA

Rapa kutoka nchini Tanzania Nikki Mbishi amesema Marioo kupitia wimbo wake “BIA TAMU” alistahili kuwa namba moja kwenye orodha ya wasanii ambao wamepata gawio la mirabaha kutoka Chama cha Hatimiliki Tanzania – COSOTA. Kupitia ukurasa wake wa Twitter Nikki mbishi amesema wimbo wa Bia Tamu umepigwa kuliko wimbo wowote nchini Tanzania katika kipindi cha miezi 7 iliyopita. “Yaani mtu unakuja na hoja jenzi ambayo pengine ingewapa hamasa Con Boi na Rapcha watu wanahisi umewalinganisha. Jamaa wapo kama COSOTA wakiulizwa vigezo vya kutoa mirabaha, hata mjinga anajua MARIOO alistahili kuwa namba moja BIA TAMU imepigwa kulizo nyimbo zote kwa 7 months ago.” alichomekea Nikki Mbishi wakati akichangia hoja kwenye tweet ya Wakazi iliyoibua mjadala mzito Twitter, tangu juzi. Kwa mujibu wa COSOTA,  Ali Kiba ndiye aliongoza kwa wasanii wa bongo fleva waliopata pesa nyingi za Mirabaha ambapo alipata kiasi cha shilling 3 za Kenya huku Marioo akikosekana hata kwenye TOP 20 ya orodha hiyo.

Read More