NINCE HENRY AFUNGUKA KUHUSU UHUSIANO WAKE NA MENEJA CHAGGA
Msanii Nince Henry kutoka Uganda amekanusha kuingia kwenye ugomvi na meneja wake wa zamani Chagga. Hii ni baada ya madai kusambaa mtandaoni kuwa wawili hao hawana maelewano mazuri kutokana na ugomvi wa pesa. Katika mahojiano yake hivi karibuni Nince Henry amesema madai hayo hayana ukweli wowote kwa sababu bado anafanya kazi na Chagga. Chagga ambaye alimtambulisha nince henry kwenye muziki anajianda kuachia album yake ya kwanza baada ya kufanya kazi ya kuwasimamia wasanii kwa miaka mingi.
Read More