Nonini Akosolewa Mitandaoni kwa Mtindo Wake Mpya wa Uimbaji

Nonini Akosolewa Mitandaoni kwa Mtindo Wake Mpya wa Uimbaji

Msanii mkongwe wa muziki wa Genge, Nonini, anakumbwa na ukosoaji mkali mitandaoni baada ya kupakia video ya nyuma ya pazia (behind-the-scenes) ya wimbo mpya kutoka kwenye albamu yake inayotarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni. Video hiyo, iliyochapishwa kwenye mtandao wa X (zamani Twitter), ilimuonesha Nonini akiwa studio akiimba kwa mtindo wake wa kipekee wa Genge huku akijaribu kuuchanganya na ladha za kisasa. Katika video hiyo, Nonini anasikika akitoa mistari inayogusia maisha yake jijini Nairobi na changamoto alizopitia akiwa ughaibuni. Aliandika kwenye chapisho hilo kuwa wimbo huo ni wa mwisho katika albamu yake mpya, na kwamba muziki kwake ni taswira ya maisha yake binafsi. Hata hivyo, badala ya kupokelewa kwa shangwe, video hiyo ilisambaa kwa kasi kutokana na mtindo wake wa uimbaji ambao wengi waliuelezea kama wa kizamani na usioendana na ladha ya muziki wa sasa. Watumiaji wengi wa X walimkosoa wakisema kuwa licha ya heshima yake kama mmoja wa waanzilishi wa muziki wa Genge nchini, Nonini anapaswa kubadilika ili kuwavutia wasikilizaji wa kizazi kipya.

Read More
 Nonini kuiburuza mahakamani kampuni ya Synix Electronics.

Nonini kuiburuza mahakamani kampuni ya Synix Electronics.

Msanii mkongwe nchini Nonini ametangaza tarehe rasmi ya kuanza kwa kesi yake dhidi ya Kampuni moja ya Kijapani inayojishughulisha ya uuzaji wa bidhaa za kielektroniki, Synix Electronics. Nonini ambaye amekuwa Mhubiri wa somo la hakimiliki kwa wasanii wa Kenya, ameweka wazi kuwa tarehe ya kupanda kizimbani na kuanza kucharuana na Kampuni hiyo, ni Machi 23 mwaka huu. Msimamo wake ni kuwa, Hakimiliki itaheshimiwa. Kampuni hiyo ilitumia sehemu ya wimbo wa Nonini katika matangazo yao ya kibiashara mwaka jana na msanii huyo alidokeza hilo kwa kupakia kipande hicho kwenye ukurasa wake. Nonini katika malalamishi yake kipindi hicho alisema kuwa, Synix walitumia kipande cha wimbo wake ‘We Kam Tu’ pasi na kupata hakimiliki kutoka kwake.

Read More
 NONINI AFUNGUA KESI MAHAKAMANI DHIDI YA BRIAN MUTINDA

NONINI AFUNGUA KESI MAHAKAMANI DHIDI YA BRIAN MUTINDA

Mwanamuziki wa Kenya anayeishi Marekani Hubert Nakitare maarufuka kama  “Nonini” amefungulia mashtaka mwanamitandao Brian Mutinda na kampuni ya kieletroniki ya Syinix. Hii ni baada ya mwanamitandao huyo kutumia wimbo wake wa “We Kamu” kwenye matangazo ya kibiashara kwenye mitandao ya kijamii bila idhini yake. Kulingana na shtaka hilo lilofunguliwa katika mahakama ya milimani jijini Nairobi, mshatikiwa ametakiwa kufika binafsi  kortini ndani ya siku 15  au akiwa na wakili wake la sivyo hatachukuliwa hatua kali za kisheria. Utakumbuka mwezi Aprili mwaka huu nonini alitishia kumfungulia mashataka brian mutinda kwa kutumia wimbo wake bila idhini yake ambapo alitoa nafasi ya mazungumzo kati yake na kampuni ya Syinix na Brian Mutinda lakini inaonekana hatua hiyo haikuzaa matunda yoyote.

Read More
 NONINI AJIUNGA RASMI NA CHAMA CHA ASCAP YA NCHINI MAREKANI

NONINI AJIUNGA RASMI NA CHAMA CHA ASCAP YA NCHINI MAREKANI

Mwanamuziki mkongwe Nonini ameikimbia Kenya na kuamua kutafuta mapato ya muziki wake nchini Marekani. Kupitia ukurasa wake wa instagram noni ametangaza rasmi kuwa amejiunga na American Society of Composers, Authors and Publishers (ASCAP) Chama kinacholinda Hakimiliki za Waandishi wa nyimbo na Watayarishaji kikiwa na zaidi ya memba 850,000. Nonini amekuwa akiishi nchini Marekani ambapo alianzisha biashara yake ya viatu, mavazi na saa za mkononi. Wiki iliyopita alitangaza kujivua Uanachama wa Chama cha Hakimiliki ya Muziki nchini Kenya (MCSK) kwa madai ya kutoridhishwa na utenda kazi wake katika mgao wa mirabaha kwa wasanii.

Read More
 NONINI AJIONDOA KAMA MWANACHAMA WA MCSK

NONINI AJIONDOA KAMA MWANACHAMA WA MCSK

Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Nonini ametangaza kujiondoa kama mwanachama wa chama cha muziki na hakimiliki nchini MCSK. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nonini amechapisha barua inaonesha kuwa ombi lake kujitoa kama mwanachama wa chama cha muziki na hakimiliki nchini MCSK imekubaliwa huku akithibitisha kuwa hatakuwa anapokea mirabaha ya muziki wake kutoka kwa chama hicho. “Insanity is doing the same thing over and over and expecting different results. Moving on to something that actually works. 💯 #Mgenge2ru”, Ameandika Instagram. Mwaka wa 2018 Nonini alijiuzulu kama mwenyekiti wa chama inayopigania haki ya watumbuzaji nchini PRISK kwa kile kilichotajwa kuwa prisk ilikwenda kinyume na kanuni zilizowekwa na bodi ya hakimiliki nchini KECOBO. PRISK ni chama ambacho kilipewa leseni ya kuhudumu na Bodi ya hakimiliki nchini KECOBO kuhakikisha inatetea maslahi ya wasanii na watumbuizaji kupitia kazi zao za sanaa.

Read More