Noti Flow Awatuhumu Maandy na Ssaru kwa Kuiga Ubunifu Wake
Rapa wa Kenya, Noti Flow, ameibua mjadala mtandaoni baada ya kuwatupia lawama wasanii wenzake Maandy na Ssaru, akiwatuhumu kwa kuiga ubunifu wake kwenye muziki. Sakata hilo limeanza siku chache tu baada ya Noti kuachia wimbo wake mpya aliofanya na mpenzi wak, Colonel Mustafa, ambao uli-sample melody kutoka kwenye hit single ya kundi The Vultures, kundi ambalo mpenzi wake huyo alianzisha miaka ya nyuma. Hata hivyo, kufuatia ujio wa kazi hiyo, Maandy na Ssaru pia waliibuka na wimbo wao mpya unaoitwa Zetu Zetu, ambao umesample kibao maarufu Monalisa cha kundi hilo. Hatua hiyo imeonekana kumkera Noti Flow, ambaye amedai kwamba wawili hao wanajaribu kuendeleza mtindo aliouanzisha yeye mwenyewe. Kupitia mitandao ya kijamii, Noti Flow hakusita kueleza hasira zake kwa maneno makali, akiwaita Maandy na Ssaru “copycats” kwa kile alichokitafsiri kama kuiga moja kwa moja mbinu na ubunifu wake.
Read More