Catherine Kusasira Atishia Kujiondoa NRM Kufuatia Kudharauliwa na Viongozi wa Chama

Catherine Kusasira Atishia Kujiondoa NRM Kufuatia Kudharauliwa na Viongozi wa Chama

Msanii na mshauri wa Rais wa Uganda kuhusu masuala ya Kampala na wakazi wa Ghetto, Catherine Kusasira, ametishia kujiondoa ndani ya chama tawala cha NRM, akilalamikia kile alichokiita dharau na kutotambuliwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho. Kusasira amesema licha ya kujitolea kwa miaka karibu kumi kutetea chama na Rais Yoweri Kaguta Museveni, bado anakumbana na vikwazo na kudharauliwa, hasa na maafisa wa usalama na baadhi ya viongozi waandamizi wa NRM. “Nimechoka na dharau kutoka kwa baadhi ya watu ndani ya NRM. Mnathubutu kunizuia kukutana na Jenerali Nalweyiso? Nimejitolea kwa ajili ya chama, lakini ni Rais pekee anayetambua juhudi zangu. Wakati mwingine nawaza kuacha siasa kabisa,” alisema Kusasira. Msanii huyo ambaye hapo awali alitangaza nia ya kugombea kiti cha Mwakilishi wa Wanawake wa Buikwe, anaonekana kupoa kisiasa na sasa anaelekeza nguvu zake katika kukuza chama kwa njia ya ushawishi na kampeni za kijamii. Kwa sasa, Kusasira anasisitiza kuwa mchango wake unapaswa kutambuliwa na kuheshimiwa na viongozi wote wa chama, sio Rais peke yake. Kauli yake imezua mijadala mikali ndani ya chama, huku wachambuzi wa siasa wakitathmini athari za manung’uniko yake kwa taswira ya NRM miongoni mwa wasanii na vijana

Read More
 CATHERINE KUSASIRA AFUNGUKA MAZITO KUHUSU CHAMA CHA KISIASA NCHINI UGANDA NRM

CATHERINE KUSASIRA AFUNGUKA MAZITO KUHUSU CHAMA CHA KISIASA NCHINI UGANDA NRM

Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Uganda Catherine Kusasira amefunguka ya moyoni baada ya viongozi wa chama cha kisiasa nchini humo nrm kumtelekeza licha ya kutumia nguvu nyingi kuikinga kifua chama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2021. Kupitia waraka mrefu aliouandika kupitia mtandao wake wa Facebook msanii huyo, amedai kwamba yeye pamoja na wasanii wenzake hawakuthaminiwa vya kutosha kwa kazi nzuri waliyowekeza katika chama cha NRM. Kusasira  amekiri hadharani kutoridhika na wandani wa  chama cha NRM huku akifichua jinsi alivyopoteza marafiki, biashara, na mashabiki wakati akipigania chama hicho lakini cha kushangazwa mpaka sasa hajatuzwa kwa bidii yake. Hata hivyo amesema watu walioelekezwa kuwazawadi wale waliowekeza nguvu zao na kujitolea kwa ajili ya chama cha nrm wamepora pesa zote huku wakiwaacha wakiandamwa na madeni. Lakini pia Kusasira amemshauri rais Yoweri Kaguta Museveni kwamba watu anaowaamini watakuwa chanzo cha anguko lake. Ikumbukwe Catherine Kusasira sio staa wa kwanza kuwachana viongozi wa NRM ambao wamekuwa na mazoea ya kujitakia makuu kwani kipindi cha nyuma tuliwaona mastaa kama Buchaman, Full Figure, na  wengine wengi wakieleza malalamiko yao juu ya uongozi wa chama hicho.

Read More