Nurse Judy amkemea Sparky Kenya kudharau watu wenye miaka 35 wasio na magari

Nurse Judy amkemea Sparky Kenya kudharau watu wenye miaka 35 wasio na magari

Mshawishi wa mitandaoni, Nurse Judy, amemtolea uvivu mtayarishaji wa maudhui yenye utata, Sparky Kenya kufuatia video moja iliyoenea mitandaoni ambapo alionekana kuwadhalilisha watu wenye umri wa miaka 35 wanaotumia usafiri wa umma Katika video hiyo, Sparky alitoa kauli ya dhihaka kuhusu watu wazima ambao bado hawana magari binafsi na hulazimika kupanga foleni au kupigania nafasi kwenye magari ya umma. Kauli hiyo imeibua hisia kali mtandaoni huku wengi wakiona kama kejeli kwa watu wanaojitahidi kupambana na hali za maisha. Nurse Judy, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, alihoji sababu ya Sparky kuwadharau watu bila kuchokozwa. Alieleza kuwa maudhui ya aina hiyo huwaweka watu wengi, hususan wanaume, katika hali ya kujiona duni au kushindwa kimaisha kwa sababu ya hali zao za kifedha au umri. Aidha, aliongeza kuwa ni jambo la kusikitisha kuona watu wakiharakishwa au kushinikizwa kufikia mafanikio kwa kutumia vigezo vya umri badala ya kuzingatia hali halisi ya maisha inayowakabili wengi, hasa katika mazingira ya kiuchumi ya sasa. Wafuasi wengi wa Nurse Judy wamemuunga mkono, wakieleza kuwa presha ya kijamii kuhusu mafanikio imekuwa chanzo kikuu cha msongo wa mawazo, na kwamba ni muhimu kwa wachekeshaji na watayarishaji wa maudhui kufahamu uzito wa maneno yao kwa jamii.

Read More