Toxic Lyrikali Apata Baraka za Nyashinski Baada ya Mafanikio ya ‘Cartman’ YouTube
Msanii nyota wa muziki wa hip hop nchini Kenya, Nyashinski, ameonyesha wazi kuunga mkono na kubariki kazi ya rapper chipukizi Toxic Lyrikali kupitia wimbo wake mpya uitwao “Cartman”. Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Nyashinski alielezea kuvutiwa na ubunifu wa wimbo huo, akithibitisha kuwa anatambua na kuthamini kipaji cha msanii huyo anayeinukia. Kwa kutumia ushawishi wake mkubwa katika tasnia ya muziki, Nyashinski aliipa kazi ya Toxic Lyrikali msukumo wa kipekee, hatua ambayo imeibua msisimko mkubwa miongoni mwa mashabiki wa muziki wa hip hop. Kutoka kwa mashairi hadi uwasilishaji, wimbo huo umesifiwa kwa ubora wake na kuonekana kama hatua muhimu kwa msanii huyo chipukizi. Baraka kutoka kwa Nyashinski, ambaye anatambulika kama mmoja wa magwiji wa muziki wa Kenya, imechukuliwa na mashabiki na wadau wa muziki kama ishara ya matumaini kwa kizazi kipya cha wasanii. Wengi wamepongeza moyo wake wa kuinua vipaji na kuonyesha mshikamano katika kukuza muziki wa ndani. Wimbo wa Cartman unaendelea kupata umaarufu mitandaoni huku mashabiki wakimpongeza Toxic Lyrikali kwa kazi nzuri, na kumshukuru Nyashinski kwa kuonyesha mfano wa kuigwa katika kuendeleza muziki wa Kenya kwa kushirikiana na wale wanaochipuka Wimbo wa “Cartman” wa msanii Toxic Lyrikali hadi kufikia sasa, umefikisha zaidi ya 879,000 ya watazamaji kwenye YouTube tangu kuchapishwa kwake miezi saba iliyopita.
Read More