Odi wa Murang’a atuhumiwa kuiba wimbo wa Shekina Karen
Mrembo anafanya vizuri na wimbo wa “Daidai” Shekina Karen amebuika na kumtuhumu msanii Odi wa Muranga kwa kuiba ubunifu wa wimbo wake uitwao “Iende” aliouachia miezi sita iliyopita. Mrembo huyo amesema yeye ndiye wa kwanza kurekodi wimbo huo ambao alikuwa amemshirikisha Smady wa Mbogi Genje lakini alishangazwa na hatua ya Odi kuchukua mashairi pamoja na jina la wimbo wake huo bila ridhaa yake na kuutumia kwenye wimbo uitwao “Sugu Iendee” aliowashirikisha wasanii Micharazzo na Smady. Kwenye mahjiano na podcast ya KIPAWA amesema licha ya kuwasilisha lalama zake kwa msanii huyo ameingiwa na jeuri ya kutochukua simu zake, jambo ambalo anadai limeumiza sana kiasi cha kulia kila mara wimbo wake wa “Iendee” unapochezwa redioni. Hata hivyo amesema kutokana na Odi wa Muranga kumdhulumiwa haki yake amemuachia mwenyezi kwa kila kitu kwa kuwa ana uwezo wa kupishana na ambaye amekataa kumrudishia fadhila licha ya kutumia ubunifu wa wimbo wake bila makubaliano yeyote kati yao. Mpaka sasa Odi wa Muranga, Micharazo na Smady hawajajibu tuhuma zilizoibuliwa na mrembo huyo dhidi yao ila ni jambo la kusubiriwa.
Read More