Cardi B Afichua Offset Hajatoa Msaada Wowote kwa Watoto Wao kwa Miezi 8

Cardi B Afichua Offset Hajatoa Msaada Wowote kwa Watoto Wao kwa Miezi 8

Mwanamuziki maarufu wa Marekani, Belcalis Almanzar, Maarufu kama Cardi B, amefichua kuwa mzazi mwenzake na rapa wa kundi la Migos, Offset, hajatoa msaada wowote wa kifedha kwa watoto wao kwa kipindi cha miezi minane. Akiwa anajibu kauli ya Offset aliyoitoa katika mahojiano na The Breakfast Club, Cardi B alikanusha vikali madai kwamba yeye ni mzazi asiyejali, akieleza kuwa ndiye anayebeba majukumu yote ya kifamilia. Cardi alisema kuwa amekuwa akitumia hadi dola 50,000 kwa mwezi kwa ajili ya watoto wao, na kumshutumu Offset kwa kushindwa kuwajibika kama baba.  “Natumia dola elfu hamsini ($50,000) kila mwezi kwa ajili ya watoto wetu, Kutoka kwenye ada za shule, huduma za afya, chakula, usafiri, hadi walinzi binafsi. Mimi ndiye nafanya yote. Mtu aseme mimi ni deadbeat? Hapana.”, Alisema Cardi B kwa hasira. Cardi B pia alionesha wasiwasi kuhusu hali ya kiakili ya Offset, akimtaka atafute msaada badala ya kueneza tuhuma za uongo dhidi yake mitandaoni. “Nakupa pole na nafasi kwa sababu najua hauko sawa kiakili. Lakini usitumie hilo kunivunjia heshima mbele ya watoto wetu na hadhira ya dunia nzima,” aliongeza. Mgogoro huo umeibua hisia kali mitandaoni. Mashabiki wa Cardi B wamemsifu kwa uwazi wake na kujitolea kama mama, huku baadhi ya wafuasi wa Offset wakimtetea na kueleza kuwa anaweza kuwa anashughulika na changamoto za kiakili au presha kutoka kwa timu yake ya kisheria. Kauli hiyo ya Cardi B inajibu mahojiano ya hivi karibuni ambayo Offset alifanya na kipindi maarufu cha The Breakfast Club, ambapo alieleza kuwa mawakili wake walimshauri kuomba msaada wa kifedha kutoka kwa Cardi kama mkakati wa kisheria kwenye mchakato wa talaka yao. Offset alidai kuwa Cardi alitaka kila kitu katika mgawanyo wa mali, na kwamba maombi yake ni sehemu tu ya kujilinda katika taratibu za mahakama. Wawili hao, waliowana mwaka 2017, wamekuwa kwenye uhusiano wa uliojaa migogoro, na sasa wapo kwenye hatua za mwisho kukamilisha talaka yao. Wana watoto wawili pamoja Kulture Kiari na Wave Set.

Read More
 Offset Awasilisha Hati Mpya ya Talaka, Amuomba Cardi B Msaada wa Kifedha

Offset Awasilisha Hati Mpya ya Talaka, Amuomba Cardi B Msaada wa Kifedha

Rapa Offset ameibua mjadala mpya kwenye sakata lake la talaka na Cardi B baada ya kuwasilisha hati mpya mahakamani akitaka kulipwa msaada wa kifedha (spousal support) kutoka kwa mke wake wa zamani. Kulingana na ripoti mpya ya TMZ, Offset hajataja kiasi anachotaka hadharani, lakini imeelezwa wazi kuwa anahitaji malipo hayo kutoka kwa Cardi B. Hatua hii inaashiria mabadiliko makubwa katika mwelekeo wa talaka hiyo, ambayo ilianza kwa utulivu mnamo Agosti 2024 baada ya Cardi B kuwasilisha ombi la kuachana rasmi na rapa huyo. Lakini sasa, hatua ya Offset kudai msaada wa kifedha inaonyesha kuwa hana mpango wa kuondoka mikono mitupu katika mchakato huo. Licha ya ombi lake la msaada wa kifedha, Offset bado anataka malezi ya pamoja ya watoto wao watatu. Hili linaonyesha kwamba, pamoja na tofauti zao, bado anataka kuwa sehemu ya maisha ya watoto wao kwa karibu. Offset bado hajazungumza hadharani kuhusu ombi hilo jipya, lakini Cardi B alionekana kutoa ishara zisizo za moja kwa moja kupitia mitandao ya kijamii, ambapo alichapisha picha kadhaa kwenye Instagram instastory, hatua ambayo mashabiki wengi wameitafsiri kama majibu ya kimya kwa taarifa hiyo. Wakati mashabiki wakisubiri kauli rasmi kutoka kwa wawili hao, hali ya mvutano kati ya mastaa hawa wawili maarufu inaonekana kuongezeka, huku pesa na watoto vikibaki kuwa kiini cha mvutano huo wa talaka.

Read More
 OFFSET AISHTAKI LEBO YA QUALITY CONTROL MUSIC

OFFSET AISHTAKI LEBO YA QUALITY CONTROL MUSIC

Rapa Offset ameifungulia mashtaka label yake (Quality Control Group) kwa kukiuka makubaliano ambayo waliingia January mwaka 2021. Kwa mujibu wa TMZ Hip Hop, Offset alifungua shauri hilo Jana Jumanne akisema aliingia makubaliano na label hiyo, ya ufanyaji kazi za peke yake (solo deal) na alilipa pesa nzuri tu kwa ajili ya kupata haki zake kama Solo Artist. Sasa baada ya kuachia ngoma yake mpya “5 4 3 2 1” chini ya Universal Music Group, Offset anadai kwamba Quality Control Group wanajaribu kutaka kuwa wamiliki wa kazi hiyo, kitendo ambacho amekiita chuki. Kwa sasa QC wanafanya kazi na Offset kwenye makubaliano ya kundi pekee ambalo ni Migos.

Read More
 OFFSET ATOA HESHIMA KWA VIRGIL ABLOH KWA KUCHORA TATTOO YENYE SURA YAKE

OFFSET ATOA HESHIMA KWA VIRGIL ABLOH KWA KUCHORA TATTOO YENYE SURA YAKE

Rapa kutoka Marekani Offset ametoa heshima kwa marehemu Virgil Abloh ambaye alikuwa ni rafiki yake lakini pia Mshirika wake Kibiashara, kwa kuchora Tattoo yenye sura yake, ametuonesha kupitia insta story kwenye mtandao wa Instagram. Offset sio wa kwanza kufanya hivyo, Drake pia ni miongoni mwa wasanii wenye Tattoo ya Virgil Abloh ambaye alifariki November 28, 2021 kwa ugonjwa wa Saratani. Virgil Abloh alikuwa mwanamitindo maarufu nchini Marekani na Mkurugenzi wa Sanaa upande wa mavazi ya Kiume katika kampuni ya Louis Vuitton, pia mmiliki wa Kampuni ya Off-White.

Read More
 CARDI B AMZAWADI OFFSET CHEQUE YA SHILLINGI MILLIONI 226

CARDI B AMZAWADI OFFSET CHEQUE YA SHILLINGI MILLIONI 226

Wakati ukichukulia poa kumbukizi ya kuzaliwa kwa mpenzi wako, huko nchini Marekani rapa Cardi B hakuwa na jambo dogo kwa Baby Daddy wake OffSet , Hitmaker huyo wa “WAP” amemsurprise mume wake Offset kwa cheque nzito ya dollar million 2 za Kimarekani kama zawadi ya Birthday yake ambayo ilikuwa Disemba 14. Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa instagram Offset ametoa shukrani za dhati kwa mke wake Cardi B kwa zawadi hiyo ya kitofauti ambayo hakuitegemea, sambamba na kuonyesha mkoba huo pamoja na bei kupitia risiti ya manunuzi. “Wow Asante mpenzi (Cardi B). Mara nyingi unaniletea vitu vya kitofauti nakupenda na nakuheshimu sana”. Aliandika Offset kupitia ukurasa wake wa Instagram. Hii sio mara ya kwanza kwa Cardi B kumpa mumewe zawadi kubwa  kwani mwaka 2020 wakati Offset aliposherehekea kutimiza miaka 29, Cardi B alimsurprise na ndinga kali,aina ya  Lamborghini Aventador SVJ.

Read More