Okello Max Akiri Kudanganya Kuhusu Kuwa na Watoto

Okello Max Akiri Kudanganya Kuhusu Kuwa na Watoto

Msanii wa R&B na Afrobeat kutoka Kenya, Okello Max, amekiri kudanganya kuhusu kuwa na watoto, jambo ambalo kwa muda mrefu limekuwa likiwachanganya mashabiki wake. Katika mahojiano na mtangazaji Shiksha, Okello Max amefafanua kuwa watoto waliowahi kuonekana naye mara kwa mara si wake, bali ni ndugu wa mchumba wake. Hitmaker huyo wa Taya, ameeleza kuwa shinikizo la mara kwa mara kutoka kwa mashabiki na jamii lilimfanya kuamua kudanganya na kudai watoto hao ni wake, jambo ambalo sasa amelikiri halikuwa sahihi. Hata hivyo, msanii huyo amebainisha kuwa sasa ameamua kufunguka ili kuondoa dhana potofu na kuweka mambo wazi kwa mashabiki wake. Amesisitiza kuwa uongo huo ulikuwa matokeo ya shinikizo na si sehemu ya maisha yake halisi.

Read More
 Willy Paul Ampa Okello Max Ushauri Kuhusu Wanawake

Willy Paul Ampa Okello Max Ushauri Kuhusu Wanawake

Msanii nyota wa muziki wa Kenya, Willy Paul, ametoa ushauri kwa msanii Okello Max, akimtaka kuzingatia nidhamu ya maisha ili kuimarisha safari yake ya muziki. Katika ujumbe wake, Willy Paul alimpongeza Okello Max kwa kipaji chake cha kipekee, akisema ana uwezo mkubwa wa kisanaa na nafasi kubwa ya kufanikisha ndoto zake. Hata hivyo, alieleza kuwa kikwazo kikuu kwa msanii huyo ni masuala ya wanawake, akiongeza kwamba kuyashughulikia kwa umakini kutamwezesha kufika mbali zaidi katika taaluma yake. Ushauri huo umeibua maoni mchanganyiko mitandaoni, baadhi ya mashabiki wakionyesha kukubaliana na hoja ya Willy Paul kwa kueleza kuwa maisha ya usanii yanahitaji nidhamu na umakini. Wengine, hata hivyo, walichukulia kauli hiyo kama utani wa kirafiki unaodhihirisha urafiki wa karibu kati ya wasanii hao wawili. Okello Max, ambaye amejizolea umaarufu kupitia sauti yake laini na mchanganyiko wa mitindo ya R&B na afrobeat, amekuwa akipanda chati za muziki nchini kwa wimbo na kolabo mbalimbali. Mashabiki wake sasa wanasubiri kuona kama atachukua hatua kufuatia ushauri huo wa wazi kutoka kwa Willy Paul, ambaye pia amepitia changamoto nyingi katika safari yake ya muziki na mara kwa mara hujitokeza kutoa maoni kwa wanamuziki chipukizi na wenzake.

Read More
 Okello Max Aachia Albamu Mpya “Healing” Yenye Nyimbo 15

Okello Max Aachia Albamu Mpya “Healing” Yenye Nyimbo 15

Msanii maarufu wa muziki wa Kenya, Okello Max, ameachia rasmi albamu yake mpya inayokwenda kwa jina “Healing”, yenye jumla ya nyimbo 15. Albamu hiyo inajumuisha ushirikiano na wasanii mbalimbali maarufu wakiwemo Watendawili, Breeder LW, Vijana Baru Baru, Christin Bella kutoka Tanzania, pamoja na Mordecai Dexx. “Healing” inaelezwa kuwa mradi wa kipekee unaogusa maisha na mapenzi, huku Okello Max akionyesha ustadi wake wa uandishi wa mashairi, utofauti wa midundo, na ushirikiano wenye nguvu kutoka kwa wasanii wa kizazi kipya. Katika kusherehekea uzinduzi wa albamu hiyo, Okello Max atafanya tamasha maalum la kusikiliza albamu hiyo (album launch party) tarehe 12 Julai katika ukumbi wa Mass House. Hafla hiyo inatarajiwa kuvutia mashabiki, wadau wa muziki, na wasanii wenzake kwa ajili ya kusikiliza kwa mara ya kwanza nyimbo zote 15, pamoja na burudani ya moja kwa moja. Uzinduzi wa “Healing” unaonesha hatua mpya katika safari ya muziki ya Okello Max, ambaye anazidi kujikuza kama mmoja wa wasanii wabunifu na wenye ushawishi mkubwa katika tasnia ya muziki wa Afrika Mashariki. Mashabiki wake sasa wanatarajia kuona albamu hiyo ikifanya vizuri kwenye majukwaa ya muziki ndani na nje ya nchi.

Read More
 Okello Max aachia rasmi Album yake mpya

Okello Max aachia rasmi Album yake mpya

Mwanamuziki kutoka Kenya Okello Max ameachia rasmi Album yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake. Album hiyo inakwenda kwa jina la Boss ina jumla ya nyimbo 15 na bonus track moja ambapo amewashirikisha wakali kama Bassman, Bonysun, Suzanna Owiyo, Femi One, Bien Bensoul, Coster Ojwang’, Jocelina, Charisma na Watendawili. Boss Album  ina nyimbo kama  Pull Up, Nipe Nafasi, Kuwa na Wewe, Kungfu,Boss Oreo na nyingine nyingi. Boss ni Album ya kwanza kwa mtu mzima Okello Max  tangu aanze safari yake ya muziki  na inapatikana exclusive kupitia mtandao wa kupakua na kusikiliza muziki wa BoomPlay.

Read More