Omah Lay Aonya Kuhusu Mafundisho Potofu Katika Dini
Mwanamuziki maarufu kutoka Nigeria, Omah Lay, ametoa maneno ya ushauri kwa mashabiki wake, akiwataka kuzingatia maisha yao binafsi na kutafuta ukweli. Katika ujumbe wake Instagram, msanii huyo alisema wazi kuwa watu hawapaswi kuendeshwa kiholela na baadhi ya viongozi wa kidini, akiwataja kuwa “wajinga” wanaoweza kupotosha na kuondoa watu kwenye njia ya ukweli. Omah Lay alisisitiza kwamba kila mtu anapaswa kujipenda, kujitambua na kutafuta ukweli, badala ya kuishi maisha ya hofu yanayochochewa na mafundisho yasiyo na msingi. Aidha, nyota huyo wa muziki alionekana kulenga moja kwa moja tabia ya baadhi ya waumini wanaokubali kila wanachoambiwa bila kuhoji, jambo alilolieleza kama kikwazo cha maendeleo binafsi na kijamii. Kauli hii imezua hisia mseto miongoni mwa mashabiki na watumiaji wa mitandao ya kijamii. Wengine wameunga mkono wakisema ni wito wa kuamsha fikra huru na kupunguza unafiki wa kidini, huku wengine wakimshutumu kwa kutumia maneno makali dhidi ya imani.
Read More