Pastor T Mwangi: Huduma ni Wito, Sio Chanzo cha Kipato Changu

Pastor T Mwangi: Huduma ni Wito, Sio Chanzo cha Kipato Changu

Mhubiri maarufu nchini Kenya, Pastor T Mwangi, amefichua kuwa hapokei mshahara wowote kutoka kwa kanisa lake, akisisitiza kuwa ameweka mipaka kati ya huduma ya kiroho na ujenzi wa maisha yake ya kifedha. Katika mahojiano aliyoyafanya hivi majuzi, Pastor T alisema licha ya nafasi yake kama kiongozi wa kiroho, ameamua kujitegemea kifedha kwa kujihusisha na biashara na uwekezaji nje ya huduma ya kanisa. Alisema hana nia ya kubeba jina la Mungu ili kutajirika, jambo ambalo limekuwa chanzo cha ukosoaji kwa baadhi ya wachungaji wanaohusishwa na anasa na tamaa ya mali. Aidha, alieleza kuwa amepewa fursa nyingi za kujiingiza kwenye biashara haramu maarufu kama wash wash, lakini alizikataa kwa misingi ya maadili na imani yake kwa Mungu. Pastor T alisema kuwa mafanikio ya kweli yanapaswa kujengwa kwa bidii, uaminifu na maarifa, sio kwa njia za mkato au kutumia jina la kanisa kwa manufaa binafsi. Kauli yake imepongezwa na wengi mitandaoni, hasa vijana wanaomwona kama kielelezo cha uadilifu na kujituma. Pastor T amejizolea umaarufu kupitia mahubiri yake ya vijana na harakati za kuinua jamii kiroho na kijamii, huku akihubiri ujumbe wa matumaini, maadili, na kujiendeleza kimaisha kwa njia halali.

Read More
 Mr. T aonya wasanii dhidi ya kiki, Adai inaharibu soko la muziki

Mr. T aonya wasanii dhidi ya kiki, Adai inaharibu soko la muziki

Baada ya wasanii kibao kutengeneza kiki kwa ajili kukamata attention ya mashabiki wao juu ya ujio wa kazi zao, Mwimbaji aliyegeukia ukasisi Mr. T yeye anapingana na kitendo hicho kwa kusema kwamba soko la muziki linakufa kwa njia hiyo. Mr. T amefunguka na kusema kitendo cha wasanii kutengeneza kiki ili waweze kuzungumziwa katika media kuliko kazi zao inaua na kuwaharibu mashabiki kutokana na kufuatilia sana skendo za mastaa kuliko kazi zao. Akizungumza na podcast ya Presenter Ali amesema kuwa kitendo hicho kimewaharibu wasanii wachanga ambao wanataka kutoka na kufikiria kuachia kiki kwanza ili wajulikane kwa haraka na kazi zao kuweza kufika mbali. Hata hivyo amesisitiza kuwa ingawa kiki ina mchango kwenye muziki ila zifanyike kwa ustaarabu kwani inaweza kuwa shubiri pale wasanii wanapotupiana maneno machafu mtandaoni.

Read More