PENZI LA PATORAKING WA NIGERIA LAMKOSESHA USINGIZI FEMI ONE
Msanii wa muziki wa rap nchini Kenya, Femi One, ameshindwa kuficha mapenzi yake kwa nyota wa muziki wa Dancehall kutoka Nigeria, patoranking. Katika kikao cha Maswali na Majibu kupitia insta story yake kwenye mtandao wa instagram , hitmaker huyo wa ‘Utawezana” amesema anatamani kuolewa na nyota huyo wa Nigeria kwa sababu ana akili pia amekuwa akimfuatilia msanii huyo kwa muda mrefu. Hata hivyo watumiaji kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kushangaza na kauli ya rapa huyo wengi wakihoji huenda femi one ana kazi ya pamoja na patoraking hivyo anatengeneza mazingira ya kuzungumuziwa kabla ya ujio wa ngoma yao mpya. Ikumbukwe Femi one tangu apate umaarufu kwenye tasnia ya muziki hajawahi weka wazi mahusano yake y kimapenzi lakini kutokana na ujumbe wake kwenye instagram page yake, inaonekana kuwa yuko tayari kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na patoraking.
Read More