Patoranking Aitembelea Kambi ya Borussia Dortmund Florida

Patoranking Aitembelea Kambi ya Borussia Dortmund Florida

Mwanamuziki nyota kutoka Nigeria, Patoranking, leo ametembelea kambi ya mazoezi ya klabu ya Borussia Dortmund iliyoko Fort Lauderdale, Florida, Marekani. Kupitia kurasa rasmi za Borussia Dortmund, picha kadhaa zimeonesha msanii huyo akikutana na wachezaji wa timu hiyo, akisalimiana nao na kubadilishana mawazo. Uongozi wa klabu hiyo umeeleza kufurahishwa na ujio wa Patoranking, wakisema ilikuwa heshima kubwa kumpokea kambini. Dortmund kwa sasa inashiriki michuano ya FIFA Club World Cup kama mwakilishi wa bara la Ulaya. Licha ya mafanikio yake katika muziki wa Afrobeats, Patoranking pia ni mdau mkubwa wa michezo nchini Nigeria. Mchango wake umeonekana wazi kupitia juhudi za kuinua vipaji vya vijana, ikiwemo ujenzi wa uwanja wa soka kwa ajili ya maendeleo ya michezo na jamii kwa ujumla.

Read More
 Patoranking kutumbuiza kwenye Kombe La Dunia 2022 huko Qatar

Patoranking kutumbuiza kwenye Kombe La Dunia 2022 huko Qatar

Mwimbaji nyota wa muziki kutoka Nigeria, Patoranking ambaye kwa sasa anafanya vizuri na smash hit yake Kolokolo akiwa na Diamond Platnumz, anatajwa kuwa atatumbuiza kwenye Kombe La Dunia 2022 huko Qatar mwezi huu katika tamasha la FIFA Fan tarehe 28. Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Albidda Park wakati wa siku 29 za mashindano ya Kombe la Dunia na halina kiingilio. Fahamu, michuano ya Kombe la Dunia 2022 huko Qatar inatarajiwa kuanza Novemba 20 na kufikia tamati Disemba 18. Mataifa 32 yatashuka uwanjani kusaka ubingwa wa michuano hiyo mikubwa ya soka duniani.

Read More