Kajala aweka wazi matamanio ya kupata mtoto
Mwigizaji wa filamu nchini Tanzania, Kajala ameweka wazi matamanio ya kupata mtoto wa pili ikiwa ni miaka 21 tangu kuzaliwa mtoto wake wa kwanza, Paula. Kupitia insta story yake amesema hatatumia tena madawa ya kuzuia mimba ya P2. “Nafikiri sasa ni muda sahihi wa kupata mdogo wako Dada Paula. Hakuna kutumia P2 tena, niko tayari kuwa mama tena”, unasomeka ujumbe wa Kajala Frida. Aidha, kwa sasa ni wazi Kajala amehamishia uzito wa penzi lake kwa watoto, na hilo amelithibitisha kwa kumfanyia (Suprise) binti yake Paula Kauli ya Kajala inakuja wiki kadhaa baada ya kuachana na Mchumba wake, Harmonize. Ikumbukwe mtoto wa kwanza, Paula, Kajala alizaa na Prodyuza wa muziki wa Bongofleva, P Funk Majani kutoka Bongo Records, lakini walikuja wakaachana baada mahusiano kukumbwa na migogoro.
Read More