Cape Verde yaupa uwanja jina la Pele

Cape Verde yaupa uwanja jina la Pele

Serikali ya Cape Verde imekuwa nchi ya kwanza ulimwenguni kuupa uwanja wake wa Taifa jina la gwiji wa soka ulimwenguni, Pele, kama ambavyo Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino alishauri nchi wanachama kufanya hivyo. Akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga Pele Jumatatu wiki hii, Infantino alitoa rai kwa nchi wanachama wa FIFA kuupa jina la Pele moja kati ya viwanja vilivyopo katika nchi hizo kama njia ya kumuenzi. Taarifa ya serikali ya Cape Verde imesema imeamua kuupa jina la Pele uwanja wa Taifa wa nchini hiyo uliofahamika awali kama Estádio da Várzea.

Read More
 Mwili wa Pele kuagwa leo

Mwili wa Pele kuagwa leo

Mwili wa gwiji wa soka wa Brazil, Edson Arantes do Nascimento almaarufu Pele utaagwa leo ukiwa katikati ya uwanja wa klabu ya Santos wa Vila Belmiro kwa masaa 24. Mazishi ya gwiji huyo yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne katika uwanja huo unaotumiwa klabu hiyo ambayo Pele aliitumikia kwa sehemu kubwa ya maisha ya kandanda. Jeneza lake litatembezwa katika mitaa ya Santos na kupita mbele ya nyumba ya mama yake mzazi Celeste ambaye ana umri wa miaka 100.

Read More
 Pele kuagwa jumatatu nchini Brazil

Pele kuagwa jumatatu nchini Brazil

Taifa la Brazil limeanza rasmi siku tatu za maombolezo kufuatia kifo cha nguli wa soka nchini humo, Edson Arantes do Nascimento maarufu Pelé aliyefariki jana Alhamisi baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu. Shughuli ya kuuaga mwili wa marehemu itafanyika Jumatatu ijayo kwa saa 24 katikati ya uwanja wa Santos, ambako ndiyo klabu ya Pelé ya nyumbani alipoanzia kucheza soka akiwa kijana mdogo. Mazishi ya nguli huyo wa soka yanatarajiwa kufanyika kwenye Ukumbusho wa Necrópole Ecumênica, kaburi la wima huko Santos, ambako aliishi zaidi wakati wa uhai wake. Familia pekee ndiyo inatajwa itahudhuria mazishi hayo. Watu mbalimbali kutoka pande zote za Dunia wameendelea kutuma salamu zao za heshima na rambirambi kufuatia kifo cha nguli huyo wa soka.

Read More
 Mkongwe wa soka Dunia Pele afariki dunia

Mkongwe wa soka Dunia Pele afariki dunia

Gwiji la Soka Duniani Edson Arantes do Nascimento maarufu kama PELE amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82. Kifo cha mwanasoka huyo, kimethibitishwa na binti yake Kely Nascimento kwenye Instagram. Mchezaji huyo wa hali ya juu alikuwa akitibiwa saratani ya utumbo mpana tangu mwaka 2021. Pele anayetajwa kama miongoni mwa Wachezaji wa soka wa kipekee kuwahi kutokea Duniani amewahi kutwaa Kombe la Dunia mara tatu akiwa na Timu ya Taifa ya Brazil.

Read More