Pinky afukuzwa Team No Sleep kwa madai ya kuvuta Shisha

Pinky afukuzwa Team No Sleep kwa madai ya kuvuta Shisha

Msanii anayekuja kwa kasi nchini Uganda Pinky ameripotiwa kutimuliwa kwenye lebo ya muziki ya Team No Sleep kwa madai ya kutoka kimapenzi na wanaume tofauti na kuvuta shisha. Duru za kuaminika zinasema licha ya meneja wake Jeff Kiwa kumuonya kila mara kujitenga na tabia hatarishi itakayomshusha kisanaa, aliendelea kumpuuza, jambo ambalo lilifanya uongozi wa TNS kusitisha mkataba wa kufanya naye kazi. Pinky mwenye umri wa miaka 18 amekuwa chini ya Jeff Kiwa kwa takriban miaka miwili lakini hana wimbo wowote mkali kwenye maktaba yake ila bado anajitahidi kuwaaminisha mashabiki kuwa ana kipaji cha kipekee katika muziki wake.

Read More
 MWANAMUZIKI WA TEAM NO SLEEP RAHMAH PINKY AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA

MWANAMUZIKI WA TEAM NO SLEEP RAHMAH PINKY AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Rahmah Pinky ameachia rasmi album yake ya kwanza chini ya lebo ya muziki ya Team No Sleep. Album hiyo ambayo imepewa jina la Seven Teen ina jumla mikwaju 6 ya moto ambayo pinky amezifanya mwenyewe bila kumshirikisha msanii yeyote. Nyimbo ambazo zinapatikana kwenye album hiyo ya Pinky imeandikwa na wasanii Sama Sojah, Khalifa Aganaga, na Dokta Brain, huku maprodyuza kama Bushigntone, Nessim, na Chemical Beatz, wakihusika kikamilifu kwenye mapishi ya Audio. Seven Teen album ina nyimbo kama, Onyuma Okulaba,Kukwagala, SuperStar, na inapatikana exclusives kwenye majukwaa yote kupakua na kusikiliza muziki mtandaoni. Utakumbuka Rahmah Pinky mwenye umri wa miaka 17 alitambulishwa kwenye lebo ya muziki ya Team No Sleep mwishoni mwa mwaka wa 2021 kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Sheebah Karungi ambaye alizinguana vibaya na meneja wake Jeff Kiwa.

Read More
 MSANII MPYA WA TNS RAHMAH PINKY AJIBU TUHUMA ZA WIZI WA WIMBO

MSANII MPYA WA TNS RAHMAH PINKY AJIBU TUHUMA ZA WIZI WA WIMBO

Msanii mpya wa Team No Sleep Rahamah Pinky amekanusha tuhuma za kumuibia msanii chipukizi nchini Uganda Morgan Gloria wimbo wake wa Superstar. Kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni Pinky amesema meneja wake jeff kiwa alinunua wimbo huo kutoka kwa mwandishi mmoja wa nyimbo ambaye hakuweka wazi jina lake. Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 17 amemtaka Morgan Gloria kumtafuta mwandishi huyo wa wimbo wake Superstar watatue tofauti zao badala ya kuichafulia jina lebo yake ya Team No Sleep kwa tuhuma za uongo. Kauli ya Pinky imekuja mara baada ya Morgan Gloria kunukuliwa kwenye moja ya interview akidai kwamba atamfungulia mashtaka msanii huyo wa TNS kwa madai ya kumuibia wimbo wake wa superstar ambao tayari alikuwa amerekodi na lebo hiyo.

Read More