Pipi Jojo Asema Hajawahi Pata Mapenzi Kama Chief Godlove

Pipi Jojo Asema Hajawahi Pata Mapenzi Kama Chief Godlove

Msanii chipukizi kutoka Tanzania, Pipi Jojo, amegusa hisia za mashabiki baada ya kufichua kwamba hajawahi kupata upendo wa baba kama anaoupata sasa kutoka kwa Chief Godlove, ambaye amekuwa akionyesha wazi kujivunia kumlea kama mwanawe. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Pipi Jojo ameeleza kuwa katika maisha yake yote tangu kuzaliwa, hakuwahi kutegemea kama siku moja angepata nafasi ya kufurahia mapenzi ya baba. Msanii huyo, amesema kwamba hatua ya Chief Godlove kumpa nafasi kama binti yake imekuwa moja ya baraka kubwa maishani mwake, na kwamba anathamini sana uhusiano huo mpya. Binti huyo anayedaiwa kuwa na umri wa miaka 16, ameeleza kuwa anafurahia kupendwa na kutunzwa kama binti halisi, na kwamba hatamuangusha mtu ambaye amempa nafasi ambayo kwa muda mrefu hakuwahi kuipata.

Read More
 Pipi Jojo Amshangaza Baba yake Kwa Mtindo wa Kipekee wa Nywele

Pipi Jojo Amshangaza Baba yake Kwa Mtindo wa Kipekee wa Nywele

Msanii chipukizi anayezidi kuibukia kwa kasi, Pipi Jojo, amezua gumzo mtandaoni baada ya kumsuprise baba yake Chief Godlove kwa mtindo mpya wa nywele za rasta uliounganishwa na pipi aina ya lollipop, ubunifu ambao umewastaajabisha wengi. Kwa mujibu wa video iliyosambaa mtandaoni, baba yake ameonekana kufurahishwa na ubunifu wa binti yake, na hata kumuuliza kwa utani kama ana kipaji cha ziada cha ubunifu wa mitindo kutokana na ujasiri wake wa kujaribu vitu vipya. Hatua hii imeongeza mwanga zaidi kwa Pipi Jojo ambaye kwa sasa anazidi kuisukuma kwa nguvu EP yake mpya “I Want Mama Proud.” Kati ya nyimbo zilizopo kwenye EP hiyo, lead single “Chakacha” imeendelea kufanya vizuri zaidi mtandaoni, ikiwa na zaidi ya watazamaji milioni moja kwenye YouTube ndani ya muda mfupi tangu iachiwe.

Read More
 Pipi Jojo Kutua Uganda kwa Ziara ya Kutangaza EP Yake “I Want My Mama Proud”

Pipi Jojo Kutua Uganda kwa Ziara ya Kutangaza EP Yake “I Want My Mama Proud”

Msanii chipukizi kutoka Tanzania, Pipi Jojo, amefichua mipango yake ya kuanza ziara ya kimuziki nchini Uganda kwa ajili ya kutangaza EP yake mpya iitwayo “I Want My Mama Proud.” Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Pipi Jojo ameonekana akizungumza kwa simu na baba yake, Chief Godlove, akimuomba magari manne kwa ajili ya kufanikisha media tour hiyo pamoja na kuandaa dance challenge ya wimbo wake “Chakacha”, ambao video yake ina zaidi ya views milioni moja ndani ya muda mfupi. Katika mazungumzo hayo yaliyovutia mashabiki, Pipi Jojo ameonekana akideka huku baba yake akimhakikishia kumpatia magari manne ya kifahari pamoja na fedha za kutosha kufanikisha ziara hiyo, ingawa alikiri alitamani kumkodishia ndege binafsi (private jet). Billionea Chief Godlove, amemsifu binti yake kwa juhudi na nidhamu anayozionyesha katika kazi yake ya muziki, akitabiri kuwa huenda akawa msanii wa kwanza kuipatia Tanzania tuzo ya Grammy. Kwa sasa, Pipi Jojo yupo katika hatua za mwisho kukamilisha ziara yake nchini Kenya, ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa kumjenga kimataifa na kumletea mashabiki wapya kutoka mataifa mbalimbali.

Read More
 Msanii Pipi Jojo Aangua Kilio Baada ya Chief Godlove Kumkimbia

Msanii Pipi Jojo Aangua Kilio Baada ya Chief Godlove Kumkimbia

Msanii wa Chief Godlove, anayefahamika kwa jina la Pipi jojo, ameangua kilio hadharani baada ya kugundua kwamba ataanza ziara yake ya vyombo vya habari nchini Kenya bila ushirika wa meneja wake huyo maarufu. Kupitia video inayosambaa mtandaoni, Pipijojo ameonekana akibubujikwa na machozi huku Chief Godlove akimfariji na kumtia moyo kabla ya safari yake. Katika ujumbe aliouchapisha kupitia ukurasa wake wa Instagram, Chief Godlove amesema kuwa binti yake Pipi Jojo amepata mwaliko wa kwenda kwenye media tour nchini Kenya, na kwamba alitarajia kumsindikiza mwenyewe lakini alishindwa kutokana na majukumu ya kikazi. Ziara hiyo inatarajiwa kuanza wiki ijayo, ambapo Pipi jojo atazuru vituo mbalimbali vya redio na televisheni nchini Kenya kwa ajili ya kutangaza miradi yake mipya ya muziki. Ziara ya Pipijojo nchini Kenya inatazamiwa kuwa hatua muhimu katika kukuza jina lake kimataifa na kuimarisha ushawishi wa muziki wa lebo ya Chief Godlove katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Read More
 Msanii Chipukizi Pipi Jojo Aachia Rasmi EP Yake Mpya

Msanii Chipukizi Pipi Jojo Aachia Rasmi EP Yake Mpya

Msanii chipukizi wa Bongofleva Pipi Jojo ameachia rasmi EP yake mpya inayojulikana kwa jina “I Want To Make My Mama Proud”, kazi ambayo inajumuisha ngoma tano alizozifanya bila kumshirikisha msanii yeyote. EP hiyo inajumuisha nyimbo kama “Chakacha,” “With You,” “Nakupenda,” “Waite,” na “Sunrise.” Kila wimbo una ladha yake ya kipekee, ikionesha ukuaji wa kimuziki na ubunifu wa msanii huyo anayejitengenezea jina kwenye muziki wa kizazi kipya. Kwa mujibu wa Pipi Jojo, mradi huu ni wa kipekee kwani umetokana na ndoto yake ya kumfanya mama yake ajivunie mafanikio yake ya muziki kutokana na maisha magumu aliyokulia. EP “I Want My Mama Proud” inapatikana kwenye majukwaa yote ya muziki mtandaoni, ikiwemo Spotify, Boomplay, na Apple Music. Pipi Jojo ni msanii aliyeibuliwa na Chief God Love, ambaye amemkabidhi prodyuza Mr. T Touch jukumu la kumsimamia kisanaa ili kuhakikisha kipaji chake kinanawiri na kufika mbali zaidi.

Read More
 Msanii Chipukizi Pipi Jojo Kutambulisha EP Mpya Oktoba 9

Msanii Chipukizi Pipi Jojo Kutambulisha EP Mpya Oktoba 9

Msanii chipukizi anayekuja kwa kasi, Pipi Jojo, ametangaza kuwa ataachia rasmi EP yake mpya Oktoba 9 kwenye majukwaa yote ya kidigitali. Kupitia ujumbe wake, Pipi Jojo ameeleza kuwa alipata nafasi ya kukutana na Chief Godlove Billionaire kwa ajili ya kumsikilizisha kazi zake, ambapo kwa bahati nzuri alikutana pia na gwiji wa muziki wa HipHop nchini Tanzania, Chid Benz. Amesema kuwa kukutana na Chid Benz kumekuwa ni heshima kubwa kwake, kwani mbali na kupata ushauri wa kitaalamu, hakutarajia kuwa msanii mkongwe wa hadhi hiyo angekubali na kubariki kazi zake. Kwa mujibu wa Pipi Jojo, wawili hao walimsikiliza kwa makini na kumpa baraka ya kuachia rasmi kazi zake, jambo ambalo amelitaja kuwa ni hatua muhimu katika safari yake ya muziki. Ameomba mashabiki, vyombo vya habari na wadau mbalimbali wa muziki kumpa sapoti ili EP yake ipokelewe vyema sokoni na kumsaidia kusonga mbele katika ndoto yake ya kuwa miongoni mwa wasanii wakubwa nchini Tanzania.

Read More