“Kifo cha PNB Rock kimenifanya niwe muoga”- Asema Lil Baby

“Kifo cha PNB Rock kimenifanya niwe muoga”- Asema Lil Baby

Rapa Lil Baby amefunguka na kusema kuwa baada ya kupata habari za kifo cha rapa mwenzake Pnb Rock kilichotokea Septemba 12 mwaka huu, amekuwa muoga hata wa kutoka nje. Kupitia mahojiano aliyoyafanya na complex, Lil Baby amesema “Imekuwa kama simu ya kuniamsha, sio kwamba sijui kuna matukio kama hayo ila taarifa za kifo cha Pnb Rock zimenifanya niwe muoga hata wa kwenda kula kwenye migahawa mikubwa pia imenifanya niwe makini zaidi” Utakumbuka Rapa PNB Rock aliuawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia Septemba 12 kwenye tukio la uvamizi lililotokea kwenye mgahawa mmoja Jijini Los Angeles.

Read More
 RAPA PNB ROCK AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI

RAPA PNB ROCK AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI

Rapa kutoka Marekani PNB Rock ameuawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia leo kwenye tukio la uvamizi lililotokea kwenye mgahawa mmoja Jijini Los Angeles. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Jijini Los Angeles, Kelly Muniz, rapa PNB Rock mwenye umri wa miaka 30 alikuwa na mpenzi wake kwenye mgahawa huo, ambaye aliweka location kwenye picha ambayo tayari imefutwa Instagram. Inaelezwa kwamba mtu mmoja ambaye bado hajafahamika alivamia mgahawa huo akiwa na silaha na kutaka vitu kutoka kwa marehemu PNB Rock ikiwemo vito vya thamani. Lakini dakika chache baadaye mtu huyo aliishia kufyatua risasi na kumpiga rapa huyo ambaye alikimbizwa hospitali na kufariki baada tu ya kufikishwa. PNB Rock ambaye alizaliwa mwaka 1991 alitapata umaarufu kwenye muziki wa Hiphop duniani kupitia wimbo wake uitwao “Selfish” ambao ulikamata nafasi ya 51 kwenye chati ya US Billboard Hot 100. Katika kipindi cha uhai wake alifanikiwa kuachia album 2 za muziki, mixtape 5, EP moja na singo 19.

Read More